TABIA 12 ZA MATAJIRI/MAMILIONEA

Maelezo

Chanzo: Zenjishoppazz



Tarehe Iliyotolewa: 2023-01-18


Download


Kituo cha Kazi/Tukio: TANZANIA
Imetembelewa mara! 19919 ... Deadline: 2025-01-18 02:29:00

TABIA 12 ZA MATAJIRI/MAMILIONEA

Zifahamu tabia 12 za matajiri na mamilionea ambazo wanazo na wanazifanyia kazi katika Maisha yao ambazo ni tofauti na wanavyoishi masikini na watu wa kipato cha chini.

Mamilionea wengi kwa kawaida huwa hawapendi kujuilikama kama wao ni mamilionea, kupitia kitabu hichi cha Millionaire Next Door, mtunzi wa kitabu amefanya utafiti juu ya mamilionea na akatambua sifa zifuatazo.

  1. Kwa kawaida huishi Maisha, chini ya kipato wanachokipata. Zaidi ya asilimia 50% ya matajiri na mamilionea huishi chini ya kipato wanachokiingiza, kwa mfano, anaweza kuishi katika nyumba moja kwa Zaidi ya miaka ishirini ambayo ni yake mwenyewe. Sasa wewe kipato chako chote kitumie katika anasa kama hujaendelea kuwa masikini.
  2. Hutumia muda mwingi katika kupanga mipano ya kifedha. Kutengeneza bajeti ya matumizi yao ni suala la msingi katika Maisha yao. Kwani Zaidi ya 80% ya matajri huishi kwa kufuata mipangilio ya bajeti. Na sio muda mwingi kuupoteza maskani.
  3. Wao hufikiria Zaidi uhuru wao na uhuru wa kifedha, jambo hili ni muhimu kuliko kushindana nani ana pesa Zaidi. Vijana wengi hasa wa uchumi wa kati hupenda kuoneshana nani anapesa Zaidi. Wao matajiri hujihusisha Zaidi na masuala ya uwekezaji wa kifedha na si mashindano.
  4. Matajiri huamini uhuru wenye maana, ni kule mtu kuweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Siku zote unapokuwa ni mtekelezaji mkubwa wa majukumu yako jambo hilo litakupelekea katika uhuru wa kifedha na kufanikiwa.
  5. Hujiajiri wenyewe. Asilimia 75 ya mamilionea hujikita Zaidi katika kujiajiri na ujasiria mali na sio kuajiriwa, bali kwa kujituma Zaidi na kutumia muda mwinyi katika uwekezaji.
  6. Wengi wa mamilionea umri wao huwa kati ya miaka 40 na 50. Kuwa huku milionea katika umri huu huja baada ya muda mrefu wa kujituma vya kutosha katika ujana, na hatimae hupata mafanikio makubwa katika utu uzima wao.
  7. Huwa wanakuwa na akiba ya kutosha ambayo inaweza kuwahufadhi kwa miaka 15. Akiba hii imepatikana baada ya miaka mingi mno ya uhifadhi wa pesa na uwekezaji.
  8. Matajiri wengi ni wasomi. Kutokana na takwimu, ni asilimia 25 pekee ya matajiri ndio ambao hawana digirii ila wengi wao ni watu ambao wamesoma. Na ni asilimia 50% ya mamilionea wote ndo wenye digirii ya pili yaani masta.
  9. Huwekeza asilimia 25% ya kipato wanachokipata kila mwaka, jambo hili huwafanya utajiri wao kuzidi kuengezeka Zaidi na zaidi.
  10. Huwa wanawekeza kwa muda mrefu sana. Matajiri wengi huwekeza uwekezaji kwa muda mrefu sana hata kama ni mika 10 au Zaidi.
  11. Hununua vitu kulingana na mahitaji na sio starehe kama watu wengi wanavyofanya.
  12. Hutumia muda mwingi katika kuendeleza ujuzi wao na ujuzi wao katika biashara kuliko watu wa kawaida wanavyofanya kwa kutumia muda mwingi katika mamba yasiyo na faida.

Unaweza kudawnload kitabu kwa kugusa neno download hapo juu.



Download

Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English