Ifahamu Museum for the Future Dubai
Maelezo
Chanzo: Zenjishoppazz
Tarehe Iliyotolewa: 2023-02-23
IFAHAMU MUSEUM OF FUTURE DUBAI
The museum of the Future Dubai ni sehemu ya maonesho ya itikadi, huduma, na bidhaa bunifu za siku zijazo. Jumba hili la Makumbusho la siku zijazo linapatika Dubai katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Jengo hili la kihistoria lilianzishwa na taasisi ijulikanayo kama Dubai Future Foundation, na lilitarajiwa kufunguliwa mwaka wa 2021, lakini hadi kufikia Disemba yam mwaka huo wa 2021 lilikuwa bado halijakamilika. Hivyo jengo lilifanikiwa kufungulia rasmi katika mji wa Dubai huko Umoja wa Falme za Kiarabu 22 Febuari ya mwaka 2022.
Miongoni mwa malengo yake makuu ya kutengenezwa jengo hilo la makumbusho ni kukuza na kuendeleza maendeleo ya technologia na Uvumbuzi hasa katika nyanya ya robotiki na matumizi ya akili bandia (Artificial Intelligence – AI).
Historia
Muhammed bin Rashid Al Maktoum, mtawala wa Dubai, makamu wa rais, na Waziri mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), alitangaza mnamo tarehe 4, mwezi wa Machi, mwaka wa 2015, mipango ya Kuanzisha makumbusho ya baadae (Museum of the Future) ilionesha wakati wa mkutano wa viongozi mbali mbali wa serekali.
Mnamo tarehe 7 Febuari mwaka wa 2016, Muhammed bin Rashid Al Maktoum alizindua maonesho ya makumbusho ya Baadae katika mkutano wa serekali za ulimwengu wa mwaka 2016. Ilipofika tarehe 24 Aprili mwaka wa 2016, Muhammed bin Rashid alizindua mpango ujuulikanao kama the Dubai Future Foundation. Chini ya muundo huo mpya, Jumba la Makumbusho la Baadae likawa katika sehemu ya Wakfu wa Dubai Future.
Mnamo tarehe 10 Febuari 2017, hadi tarehe 9 Fubuari 2018, jumba la makumbusho la siku zijazo la Dubai likaweka kwa muda huko Madinat Jumeira wakati wa mkutano wa kilele wa serekali za ulimwenguni.
Na ilipofika tarehe 22 Febuari 22, Jumba la Makumbusho la wakati ujao (Museum of the Future) lilifunguliwa rasmi. Sherehe za ufunguzi na haki ya kufungua makumbusho hayo alipewa Sheikh Muhammed bin Rashid Al Maktoum Pamoja na Sheikh Hamdan bin Muhammed bin Rashid Al Maktoum (maarufu kwa jina la Fazza) ambae ni mwana mfalme wa Dubai.
Maonesho ya Museum of Future Dubai
Kama sehemu ya mkutano mkuu wa kilele wa Serekali za Ulimwengu, jumba la makumbusho la Dubai (Museum of Future Dubai) limefanya maonesho kadhaa tangu lilipozinduliwa mnamo mwaka 2016. Katika maonesho hayo mbali mbali yaliyokuwa yakioneshwa yalikuwa na mada tofauti tofauti zilizolenga matumizi ya teknolojia katika Nyanja mbali mbali.
Muundo wa Ujenzi wa jengo lenyewe
Jengo hili ni katika moja ya majengo yenye muundo wa kipekee na wenye kuvutia duniani. The museum of Future Dubai liliunda kwa kupitia studio ya usanifu ya Killa Design na kujengwa na Buro Happold. Sehemu ya nje ya jengo hili kuna maandishi yaliyoundwa kupitia shairi la kiarabu lililosomwa na mtawala wa Dubai ambayo yanahusu mustakbali wa Umoja wa falme za kiarabu.
Maneno yalioandikwa kwenye Jumba Hili la makumbusho ya baadae ya Dubai, ni nukuu tatu kutoka katika shairi la Sheikh Muhammed bin Rashid Al Maktoum, kama ifuatavyo.
- "Hatutaishi kwa mamia ya miaka, lakini tunaweza kuunda kitu ambacho kitadumu kwa mamia ya miaka".
- "Wakati ujao utakuwa kwa wale ambao wataweza kufikiria, kubuni na kuijenga, siku zijazo hazisubiri, siku zijazo zinaweza kubuniwa na kujengwa leo"
- "Siri ya Maisha mapya, maendeleo ya ustaarabu na maendeleo ya ubinadamu iko kwa neno moja tu: uvumbuzi"
Nukuu za maandishi ya Kiarabu kwenye Jumba la Makumbusho ya Wakati Ujao huko Dubai zimeandikwa na msanii wa Imarati Matar Bin Lahej. Jumba la kumbukumbu (museum of the Future of Dubai) lina horofa saba zilizowekwa kwa ajili ya maonyesho tofauti tofauti.
Horofa tatu za mwanzo zimewekwa kwa ajili ya ukuzaji wa rasilimali ya anga za juu, mifumo ya ikolojia, uhandisi wa viumbe hai, afya na ustawi wa jamii. Ghorofa nyingine zilizobakia zinaonyesha teknolojia za hivi karibuni ambazo hushughulikia changamoto katika maeneo mbali mbali ikiwa ni pamoja na afya, maji, chakula, usafiri na nishati, huku ghorofa ya mwisho ikiwa ni maalum kwa ajili ya watoto.
Jumba la makumbusho la baadae la Dubai lina maabara za uvumbuzi zinazotolewa na sekta mbali mbali, ikiwa ni pamoja na afya, elimu, miji, nishati na usafiri. Pia itasaidia katika uvumbuzi mpya kwa kushirikiana na taasisi za utafiti na vyuo vikuu mbali mbali ulimwenguni.