NAFASI ZA KAZI WIZARA YA UJENZI MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI
Maelezo
NAFASI ZA KAZI WIZARA YA UJENZI MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Ukama ifuatavyo:-
1. Afisa Utumishi Msaidizi Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
- Awe ni Mzanzibari.
- Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya ‘Human Resource Management’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
2. Mtunza Ghala Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
- Awe ni Mzanzibari.
- Awe amehitimu elimu ya ‘Stashahada’ katika fani ya ‘Store Keeper’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
3. Mlinzi Daraja la III “Nafasi 2” Unguja na “Nafasi 10” Pemba
Sifa za Waombaji:
- Awe ni Mzanzibari
- Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya Ulinzi (JKU na Mgambo).
4. Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 1” Unguja na “Nafasi 2” Pemba
Sifa za Waombaji:
- Awe ni Mzanzibari.
- Awe amehitimu elimu ya ‘Stashahada’ katika fani ya ‘Record Management’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
5. Fundi Seremala Daraja la III “Nafasi 2”
Sifa za Waombaji:
- Awe ni Mzanzibari.
- Awe amehitimu elimu ya ‘Cheti’ katika fani ya ‘Capentre’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
6. Dereva Daraja la III “Nafasi 1” Unguja na “Nafasi 2” Pemba
Sifa za Waombaji:
- Awe ni Mzanzibari
- Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata leseni ya Udereva Class ‘C’ iliyotolewa Zanzibar
7. Taarish Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
- Awe ni Mzanzibari
- Awe amehitimu Elimu ya Sekondari.
8. Muhudumu Daraja la III “Nafasi 1” Unguja na “Nafasi 2” Pemba
Sifa za Waombaji:
- Awe ni Mzanzibari
- Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya uhudumu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
9. Mfungua Maji Daraja la III “Nafasi 2” Pemba
Sifa za Waombaji:
- Awe ni Mzanzibari
- Awe amehitimu Elimu ya Sekondari au Veta.
10. Fundi Umeme Daraja la III “Nafasi 2” Pemba
Sifa za Waombaji:
- Awe ni Mzanzibari.
- Awe amehitimu elimu ya Stashahada, au FTC au Veta kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
11. Fundi Mwashi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
- Awe ni Mzanzibari
- Awe amehitimu Elimu ya Sekondari.
12. Karani Mapato Daraja la III “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
- Awe ni Mzanzibari.
- Awe amehitimu elimu ya ‘Stashahada’ katika fani ya ‘Accounting’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
13. Fundi Mchundo Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
- Awe ni Mzanzibari.
- Awe amehitimu elimu ya Stashahada, au Veta katika fani ya ‘Majengo’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
14. Mkaguzi wa Magari Daraja la II “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
- Awe ni Mzanzibari.
- Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Injinia wa Magari kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
15. Waziba Mpira Daraja la III “Nafasi 2” Pemba
Sifa za Waombaji:
- Awe ni Mzanzibari.
- Awe amehitimu elimu ya ‘Cheti’ au Veta kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
16. Afisa Utumishi Daraja la II “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
- Awe ni Mzanzibari.
- Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza’ katika fani ya ‘Human Resource Management’ au ‘Public Administration’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jinsi ya Kuomba:
- Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.
• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 17 Julai, 2017 wakati wa saa za kazi