Nafasi ya Kazi Mhandisi Umeme (Electrical Engineer) Daraja la II-UNGUJA - 1 Post

Maelezo

Chanzo: Zan Ajira



Tarehe Iliyotolewa: 2024-03-31



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 8915 ... Deadline: 2024-04-12 15:30:00

POSTMhandisi Umeme (Electrical Engineer) Daraja la II-UNGUJA - 1 POST
EMPLOYEROFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI (CAG)
APPLICATION TIMELINE:From: 27-03-2024 To: 12-04-2024
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
  • Kukagua mifumo ya umeme na kufanya matengenezo madogo madogo katika majengo ya Serikali
  • Kufanya ukaguzi wa usanifu wa miradi mbali mbali ya umeme
  • Kukagua na kusimamia hali ya ufungaji mashine katika taasisi za Srikali
  • Kufanya kazi ya kutengeneza mitambo na mifumo ya umeme ya Ofisi
  • Kufanya Ukaguzi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali ikiwemo na miradi mbalimbali ya umeme
  • Kusaidia katika kutambua maeneo yanayoweza kufanyiwa Ukaguzi pamoja na kutunza na kuhifadhi taarifa mbalimbali juu ya Ukaguzi
  • Kusaidia katika uandaaji wa mipango kazi ya Ukaguzi
  • Kusaidia katika kuandaa ripoti ya utafiti wa awali pamoja na Mipango ya Kazi itakayosaidia katika kufanya Ukaguzi
  • Kukusanya taarifa na nyaraka za ukaguzi kwa ajili ya kufanya Ukaguzi
  • Kusaidia katika kuchakata taarifa na kuandaa ripoti za Ukaguzi
  • Kusaidia katika kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo ya Kaguzi zilizokwishafanyika
  • Kusaidia katika uandaaji wa taarifa za ufuatiliaji wa mapendekezo ya Ukaguzi
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi zinazoendana na sifa na fani yake.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE
  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika  fani ya Uhandisi Umeme kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na awe amesajiliwa na Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB).
  • Awe na umri usiozidi miaka 46
  • Barua za maombi ziwasilishwe na mambo yafuatayo:-
  • Maelezo binafsi ya muombaji (CV).
  • Vivuli vya vyeti vya kumalizia masomo na kwa aliyesoma nje ya Tanzania anatakiwa kuambatanisha kivuli cha cheti cha uthibitisho kutoka TCU.
  • Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
  • Kivuli cha kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.
  • Picha ya rangi ya muombaji ya karibuni (Current Colored Passport Size Picture).
REMUNERATIONZPSJ-01

Click Here to Apply for this Post



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2025 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English