Nafasi ya Kazi Mkadiriaji Majengo (Quantity Surveryor) Daraja la 11 Unguja

Maelezo

Chanzo: Zan Ajira



Tarehe Iliyotolewa: 2024-08-13



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 4321 ... Deadline: 2024-08-24 15:30:00

POSTMkadiriaji Majengo (Quantity Surveyor) Daraja la II -UNGUJA - 1 POST
EMPLOYEROFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI (CAG)
APPLICATION TIMELINE:From: 13-08-2024 To: 24-08-2024
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
  1. Kufanya kazi kama Mkaguzi wa Ufanisi na kuwa na jukumu la kufanya Kaguzi za Ufanisi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali ikiwemo programu na miradi mbalimbali ya maendeleo katika  ukadiriaji na uthamini wa majengo.
  2. Kusaidia katika kutambua maeneo yanayoweza kufanyiwa Ukaguzi wa ufanisi kwa kuweza kukadiria majengo yanayojengwa kupitia miradi mbali mbali pamoja na kutunza kumbukumbu na taarifa za miradi hiyo.
  3. Kusaidia katika uandaaji wa mipango kazi ya Kaguzi za Ufanisi kuhusiana na miradi ya ujenzi na kufanya tathmini ya majengo.
  4. Kusaidia katika kuandaa ripoti ya utafiti wa awali pamoja na Mipango ya Kazi itakayosaidia katika kufanya ukaguzi wa ufanisi.
  5. Kukusanya taarifa na nyaraka za ukaguzi kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa ufanisi kuhusu ukadiriaji wa majengo.
  6. Kusaidia katika kuchakata taarifa na kuandaa ripoti za ujumla za ukaguzi wa ufanisi kuhusu tathmini ya majengo.
  7. Kusaidia katika kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo ya kaguzi za ufanisi zilizofanyika.
  8. Kusaidia katika uandaaji wa taarifa za ufuatiliaji wa mapendekezo ya kaguzi za ufanisi; pamoja na
  9. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na msimamizi wake.

 

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe na Shahada/Stashahada ya Juu ya kuhusiana na uhandisi wa ukadiriaji wa majengo Uhandisi (Bachelor of Science in Building Economics, Bachelor of Science in Quantity Surveying and Construction Economics) au fani nyengine zinazoshabihiana moja kwa moja  na fani hizo kutoka katika Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
  • Awe na umri usiozidi miaka 46
  • Barua za maombi ziwasilishwe na mambo yafuatayo:-
  • Maelezo binafsi ya muombaji (CV).
  • Vivuli vya vyeti vya kumalizia masomo na kwa aliyesoma nje ya Tanzania anatakiwa kuambatanisha kivuli cha cheti cha uthibitisho kutoka TCU.
  • Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
  • Kivuli cha kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.
  • Picha ya rangi ya muombaji ya karibuni (Current Colored Passport Size Picture).
REMUNERATIONZPSJ-01

BOFYA HAPA KUFANYA MAOMBI



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English