Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Daraja la II-PEMBA - 1 POST
Maelezo
Chanzo: zan ajira
Tarehe Iliyotolewa: 2025-08-16
Kituo cha Kazi/Tukio: PEMBA
Imetembelewa mara! 1914 ... Deadline: 2025-08-30 15:30:00
POST DETAILS
POST | Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Daraja la II-PEMBA - 1 POST |
---|
EMPLOYER | ZANZIBAR FOOD AND DRUG AGENCY (ZFDA) |
---|
APPLICATION TIMELINE: | From: 16-08-2025 To: 30-08-2025 |
---|
DUTIES AND RESPONSIBILITIES | Majukumu: - Kusaidia katika usanidi, usasishaji na uendeshaji wa mifumo ya kompyuta ya ZFDA;
- Kufuatilia utendaji wa mifumo na kuripoti matatizo kwa ngazi ya juu;
- Kutoa msaada kwa watumiaji kuhusu matumizi ya mifumo ya kiutawala na kiufundi;
- Kusaidia katika kuweka hatua za usalama wa mifumo ya TEHAMA;
- Kufanya matengenezo ya kawaida (routine maintenance) ya mifumo;
- Kutunza kumbukumbu sahihi za usanidi na mabadiliko ya mfumo;
- Kusaidia katika utekelezaji wa sera na taratibu za TEHAMA;
- Kushiriki katika mafunzo na kuboresha ujuzi kuhusu mifumo mbalimbali ya taasisi;
- Kusaidia katika kusimamia tovuti za taasisi;
- Kutunza nyaraka za mifumo ya TEHAMA na taratibu zake;
- Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo mwaka, nusu mwaka na mwaka.
- Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake.
|
---|
QUALIFICATION AND EXPERIENCE | Sifa za Muombaji: - Awe ni Mzanzibari.
- Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘TEHAMA kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
- Awe na uzoefu wa kusimamia na kutumia mifumo ya kielektroniki pamoja na miradi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inayohusiana na mifumo.
- Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.
|
---|
REMUNERATION | ZPSH-10 |
---|
Share via Whatsapp