Nafasi za Kazi BAKITA
Maelezo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb.Na.JA.9/259/01/A/109 14 JUNI, 2022 TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Kwa niaba ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na Wakala wa Chuo ch Taifa cha Utalii (NCT), Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi Wa Umma anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi tatu (3) kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.
1.0BARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA (BAKITA)
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ni Taasisi ya Umma ambayo iko chini ya Wizara yenye dhamana ya utamaduni. Baraza liliundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 27 ya mwaka 1967 na marekebisho yake. Kutokana na Sheria hii Baraza ndilo Wakala wa Serikali lenye mamlaka ya kusimamia na kuratibu shughuli za wadau wote wanaokuza Kiswahili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, Baraza ni mdau muhimu wa maendeleo ya Kiswahili kimataifa.
TAFADHALI PAKUA FAILI LA PDF HAPA KUPATA MAELEKEZO ZAIDI