Nafasi za Kazi Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana

Maelezo

Chanzo: Utumishi Zanzibar



Tarehe Iliyotolewa: 2019-06-06



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 11836 ... Deadline: 2019-06-07 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana kama ifuatavyo:-

1. Afisa Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Daraja la II “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Habari na Mawasiliano kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Bwana/Bibi Shamba Daraja la III “Nafasi 1” Pemba 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada ya Kilimo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Tarishi Daraja la III “Nafasi 1” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. 

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 07 Juni, 2019 wakati wa saa za kazi



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English