Nafasi za Kazi MDA na LGA
Maelezo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/ K/270 27
Agosti, 2020
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi kumi na mbili (12) kama zilivyoainishwa hapa chini.
1. FUNDI SANIFU MSAIDIZI (MAJI) – NAFASI 1
Kituo cha kazi atakachopangiwa: Halmashauri ya Manispaa ya Musoma
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kupima uwingi wa maji mtoni
ii. Kusoma kituo cha hali ya hewa
iii. Kufanya utafiti wa maji chiniya ardhi
iv. Kuchora michoro ya utafiti wa maji chini ya ardhi
v. Kukusanya sambupili za udongo zilizopatikana wakati wa uchimbaji.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliiohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachotambulika na Serikali ambao wana cheti cha ufundi Daraja la III,
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS. A