Nafasi za Kazi MKURABITA
Maelezo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/ J/252 07 Februari, 2019
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa wa kujaza nafasi za kazi mbili (2) kama zilivyoainishwa kwenye tangazo hili.
1.0 MPANGO WA KURASIMISHA RASILIMALI NA BIASHARA ZA WANYONGE
TANZANIA (MKURABITA)
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania maarufu kama “MKURABITA” ni miongoni mwa jitihada za serikali katika kuwezesha jamii kiuchumi. MKURABITA imeanzishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 2004 kwa lengo la kuwapa nguvu ya kiuchumi wananchi kwa kuwaongezea uwezo wa kumiliki na kufanya biashara katika mfumo rasmi unaozingatia utawala wa sheria. Mpango huu unasimamiwa na kuratibiwa na Ofisi ya Rais, Ikulu.
MKURABITA ni sehemu ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA) na Mkakati wa Kuondoa Umasikini Zanzibar (MKUZA), ukilenga kuwawezesha walengwa kutumia rasilimali na biashara zao zilizo rasimishwa katika kujipatia mitaji, soko pana na fursa zingine zinazopatikana katika sekta rasmi na hivyo kupunguza umaskini wa kipato.