Nafasi za Kazi Mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na nishati Zanzibar (ZURA)
Maelezo
MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA MAJI NA NISHATI ZANZIBAR (ZURA)
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA), imeanzishwa chini ya Sheria Namba 7 ya 2013 ikiwa na jukumu la kusimamia huduma za Maji na Nishati hapa Zanzibar.
ZURA kwa uwezo na mamlaka iliyonayo chini ya Kifungu Nambari 16 (c) ya Sheria Namba 7 ya 2013 inawatangazia wananchi wenye sifa, kuomba nafasi za ajira kama zifuatazo katika Afisi zake za Unguja na Pemba.
1. Afisa Manunuzi na Ugavi Mkuu Daraja la Kwanza – Nafasi 1 Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe na Shahada ya Kwanza au Shahada ya Uzamili ya Manunuzi na Ugavi au fani inayolingana na hiyo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitano (5), miaka mitatu (3) kati ya hiyo awe ametumikia katika nafasi anayoiomba.
• Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
2. Mkaguzi Nishati Mafuta Daraja la Pili – Nafasi Mbili, 1 Unguja na 1 Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Kuajiriwa mwenye Shahada ya kwanza katika fani za Nishati ya Mafuta, gesi au inayolingana na hizo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
3. Mchumi/Mchambuzi Fedha Daraja la Pili – Nafasi 1 Unguja. Sifa za Muombaji:
• Awe na Shahada ya Kwanza ya Uchambuzi wa fedha (Financial Analysis) Uchumi (Economics), Mipango ya Uchumi (Economic Planning) au fani inayolingana na hizo kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na ujuzi mkubwa katika matumizi ya kompyuta.
4. Afisa Mtatuzi wa Migogoro Daraja la Pili. Nafasi 1 Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe na Shahada ya Kwanza ya Utatuzi wa Migogoro, Sheria, Ustawi wa Jamii au fani inayolingana na hizo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
• Awe amefanya mafunzo ya vitendo ya Sheria (Legal Internship)
5. Afisa Utawala Daraja la Pili – Nafasi 1 Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe na Shahada ya Kwanza ya Utawala wa Umma, Rasilimali Watu au fani inayolingana na hizo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta na utunzaji wa kumbukumbu.
6. Afisa Usalama na Mazingira Daraja la Pili. Nafasi 1 Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe na Shahada ya Kwanza katika fani ya Sayansi ya Mazingira/Afya na Usalama au fani inayolingana na hizo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
TAARIFA ZA JUMLA
• Muombaji atakaechaguliwa kufanya usaili, usaili huo utafanyika katika katika ukumbi ambao Mamlaka itaamua na kuwataarifu waombaji.
• Muombaji atakaefanikiwa kuajiriwa anatakiwa awe tayari kufanya kazi katika Afisi yoyote ya ZURA ya Unguja na Pemba.
• Muombaji anatakiwa asiwe muajiriwa wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe tayari kufanya kazi yoyote atakayopangiwa na Mamlaka.
• Muombaji anatakiwa awe Mzanzibari.
TAREHE YA MWISHO WA MAOMBI
Maombi yataanza kupokelewa kuanzia leo tarehe 10/04/2018 na mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 14/04/2018.
NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI
Waombaji wote wanatakiwa kuwasilisha barua za maombi zilizoandikwa kwa mkono, katika Afisi za Kuu ya ZURA na kuambatanisha na vivuli vya taarifa zifuatazo:
1) Vyeti vya kumalizia masomo
2) Maelezo Binafsi (CV)
3) Cheti cha kuzaliwa
4) Picha mbili za paspoti zilizopigwa karibuni
5) Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi
Maombi yote yawasilishwe katika anuani ifuatayo:
MKURUGENZI MKUU,
MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA MAJI NA NISHATI (ZURA),
S.L.P 2238, GHOROFA YA PILI, JENGO LA MFUKO WA BARABARA, MAISARA, ZANZIBAR.
ANGALIZO
KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSIANA NA TANGAZO HILI, FUATILIA KATIKA TOVUTI YA ZURA www.zura.go.tz AU TUME YA UTUMISHI SERIKALINI NA GAZETI LA ZANZIBAR LEO.