Nafasi za Kazi Manispaa ya Bukoba

Maelezo

Chanzo: Utumishi Tanzania



Tarehe Iliyotolewa: 2020-05-08


Download


Kituo cha Kazi/Tukio: Tanzania
Imetembelewa mara! 42837 ... Deadline: 2020-05-20 15:30:00

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI 

 

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba kupitia Kibali cha Ajira Mbadala kilichotolewa na Katibu Mkuu, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa barua Kumb. Na.FA.170/368/01101 ya tarehe 31 Machi, 2020 anawatangazia watanzania wote wenye sifa za kuajiriwa kuleta maombi yao ya nafasi za kazi kama ifuatavyo:- 

 

1. MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III (TGS B) - NAFASI 2 

 

A: SIFA ZA MWOMBAJI: 

 

i) Aliyefaulu elimu kidato cha nne (IV) au sita (VI) 

ii) Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: - Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali. 

 

B: MAJUKUMU MTENDAJI WA MTAA III: 

 

i) Atasimamia utekelezaji wa Sera za Halmashauri; 

ii) Ataishauri Kamati ya Mtaa kuhusu mipango ya maendeleo ya Mtaa; 

iii) Atasimamia utekelezaji wa sheria ndogo pamoja na sheria nyingine zinazotumika katika eneo la Mtaa; 

iv) Ataishauri Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya ulinzi na usalama; 

v) Atasimamia utekelezaji wa mikakati mbali mbali inayohusu uondoaji wa njaa na umaskini; 

vi) Atakuwa Afisa Mhasibu wa Kamati ya Mtaa; 

vii) Ataandaa na kutunza Rejesta ya wakazi wote wa mtaa; 

viii) Atakuwa msimamizi wa wataalam wanaofanya kazi katika Mtaa; 

 

TAFADHALI PAKUA FAILI LA PDF KUPATA MAELEZO ZAIDI

 



Download

Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English