Nafasi za Kazi Manispaa ya Morogoro

Maelezo

Chanzo: Utumishi Tanzania



Tarehe Iliyotolewa: 2020-05-05


Download


Kituo cha Kazi/Tukio: Morogoro
Imetembelewa mara! 36110 ... Deadline: 2020-05-11 15:30:00

TANGAZO LA KAZI 

 

Kwa mujibu wa Kibali cha Ajira Mbadala kilichotolewa na Katibu Mkuu – Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro chenye Kumb. Na. FA. 170/361/01/209 cha tarehe 01 Aprili, 2020 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro anawatangazia watanzania wenye sifa na ujuzi stahiki kujaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:- 

 

MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III - NAFASI 11 SIFA ZA MWOMBAJI: 

 

Awe mwenye Elimu ya Kidato cha nne au sita na aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika mojawapo ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali. 

 

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III: 

 

(i) Katibu wa Kamati ya Mtaa 

(ii) Mtendaji Mkuu wa Mtaa 

(iii) Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Mtaa 

(iv) Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Mtaa (v) Msimamizi wa utekelezaji wa Sheria Ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika katika Mtaa 

(vi) Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama 

(vii) Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na umaskini katika Mtaa 

(viii) Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote 

(ix) Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mtaa na 

(x) Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata 

 

NGAZI YA MSHAHARA 

 

Kwa mujibu wa Ngazi ya Mshahara wa Serikali, yaani TGS B kwa mwezi. 

 

MASHARTI YA JUMLA KWA MWOMBAJI: 

1. Mwombaji awe Raia wa Tanzania na awe tayari kufanya kazi kwenye Mtaa wowote ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro. 

2. Mwombaji awe na umri kati ya miaka 18 - 45. 

3. Mwombaji awe hajawahi kupatikana na kosa la jinai au kufungwa jela. 

4. Maombi yote yaambatane na Wasifu wa mwombaji (CV). 

5. Maombi ya ambatanishwe na nakala za vyeti vya elimu, vyeti vya taaluma, cheti cha kuzaliwa na picha (passport size) zilizoandikwa jina la mwombaji nyuma. 

6. Testimonials “Provisional Results”, “Results Slips”, Kiapo cha kuthibitisha umri wa kuzaliwa HAVITAKUBALIWA. 

7. Barua ya maombi iandikwe kwa mkono. 

8. Waombaji ambao walisoma nje ya nchi vyeti vyao vya Taaluma vifanyiwe ulinganishi na TCU na NECTA na majibu ya ulinganisho yaambatanishwe kwenye barua ya maombi ya kazi. 

9. Waombaji waliowahi kuacha kazi, kuachishwa au kufukuzwa kazi hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama ana Kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi cha kuajiriwa tena. 

10. Mwisho wa kupokea maombi ya kazi ni tarehe 11/05/2020 saa 9.30 Alasiri. 

11. Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta kwa:- 

 

MKURUGENZI WA MANISPAA, HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO, S.L.P 166, MOROGORO. 

 

Sheilla E. Lukuba 

 

MKURUGENZI WA MANISPAA MOROGORO 

 

Tangazo hili pia linapatikana kwenye:- 

 

1. Tovuti ya Halmashauri ya Manispaa – www.morogoro.go.tz.



Download

Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English