Nafasi za Kazi Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
Maelezo
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Wazanzibari wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi nane (8) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.
1.0 OFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI ZANZIBAR (OCAGZ)
Kifungu cha 112 (3) cha Katiba ya Zanzibar kinampa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali jukumu la kuhakikisha kwamba fedha zote zinazokusudiwa kutolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar matumizi yake yameidhinishwa kisheria na iwapo atatosheka kwamba masharti hayo yatatekelezwa ipasavyo, basi ataidhinisha fedha hizo zitolewe.
Vile vile Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ana jukumu la kuhakikisha kwamba fedha zote ambazo matumizi yake yameidhinishwa yanatokana na fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Mapinduzi au fedha ambazo matumizi yake yameidhinishwa na Sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi, na ambazo zimetumika kwa ajili ya shughuli zilizohusika na matumizi ya fedha hizo na kwamba matumizi hayo yamefanywa kwa kufuata idhini iliyotolewa kuhusu matumizi hayo; na
Kifungu cha 112(5) cha Katiba ya Zanzibar kinaeleza kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atawasilisha kwa Rais kila taarifa atakayotoa kwa mujibu wa masharti ya kijifungu cha (3) (c) cha kifungu hiki. Baada ya kupokea taarifa hiyo Rais atawaagiza watu wanaohusika wawasilishe taarifa hiyo kwenye kikao cha kwanza cha Baraza la Wawakilishi kitachofanyika baada ya Rais kupokea taarifa hiyo na itabidi iwasilishwe katika kikao hicho kabla ya kupita siku saba tangu siku ile kilipoanza kikao hicho. Iwapo Rais hatachukua hatua za kuwasilisha taarifa hiyo kwenye Baraza la Wawakilishi, basi Mdhibiti