Nafasi za Kazi Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Zanzibar

Maelezo

Chanzo: Utumishi Zanzibar



Tarehe Iliyotolewa: 2020-06-22



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 51289 ... Deadline: 2020-06-30 15:30:00

Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Zanzibar, imeanzishwa chini ya sheria Nam.10/2011 ikiwa na jukumu la kutoa huduma za kiuchunguzi na kudhibiti kemikali kwa kuweka usalama wa afya za binaadam na mazingira. 

 

Wakala wa Maabara ya Mkemia kwa uwezo uliyonayo chini ya kifungu nambari 12 (1)-(2) ya sheria Nam. 10/2011 inapenda kuwatangazia wananchi wenye sifa kujaza nafasi za ajira kama zifuatazo katika Afisi zake za Unguja na Pemba.

 

 1. MICROBIOLOGIST DARAJA LA II. 

Nafasi 3 Unguja 

 

Sifa za Muombaji: 

? Awe Mzanzibari 

? Awe na Shahada ya kwanza katika fani ya Microbiology au applied microbiology kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 ? Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

? Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada. 

 

2. MOLECULAR BIOLOGIST/GENETIC DARAJA LA II.

 Nafasi 3 Unguja. 

Sifa za Muombaji: 

? Awe Mzanzibari 

? Awe na Shahada ya kwanza katika fani ya Genetics na biochemistry, Molecular Biology, Molecular Biology na Biotechnology au inayolingana na hizo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

? Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

? uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada 

 

3. MKEMIA (CHEMIST) DARAJA LA II. 

Nafasi 1 UNGUJA na Nafasi 2 PEMBA 

 

Sifa za Muombaji: 

? Awe Mzanzibari 

? Awe na Shahada ya kwanza Chemistry, forensic Toxicology, Forensic Science kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

? Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

? Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada 

 

4. PETROLIUM CHEMIST DARAJA LA II. 

 

Nafasi 1-Unguja 

 

Sifa za Muombaji. 

 

? Awe Mzanzibari 

? Awe na Shahada ya kwanza ya Petrolleum Chemistry au fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

? Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

? Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada. 

 

5. BIO - ENGINEER DARAJA LA II. 

Nafasi 1 UNGUJA. 

 

Sifa za Muombaji: 

? Awe Mzanzibari 

? Awe na Shahada ya kwanza ya Bioinstrumentation, Biomechanics, Clinical engineering, au fani inayolingana kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

? Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

? Awe na uwezo wa kubuni na kutambua mahitaji sahihi ya huduma ya vifaa inayohitajika. 

? Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada. 

 

TAARIFA ZA JUMLA 

 

Kwa waombaji wote watakaopata bahati ya kuchaguliwa kutafanyika usaili katika ofisi za Mkemia Mkuu zilizopo Maruhubi Zanzibar.  

 

Muombaji yeyote atakaechaguliwa anatakiwa awe tayari kufanya kazi yoyote atakayo pangiwa kuhusiana na fani yake ndani ya maabara. 

 

TAREHE YA MWISHO WA MAOMBI 

 

Maombi yataanza kupokelewa kuanzia tarehe 22/06/2020 na tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 30/06/2020. 

 

NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI 

 

Waombaji wote wanatakiwa kuwasilisha barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono katika ofisi za Wakala wa Maabara- Maruhubi Unguja na kwa Upande wa Pemba ofisi ya Mkemia Mkuu Madungu na kuambatanisha na vivuli vya taarifa zifuatazo; 

1. Vivuli vya Vyeti vya kumalizia masomo 

2. Maelezo Binafsi (CV) 

3. Cheti cha kuzaliwa 

4. Picha mbili za paspoti zilizopigwa karibuni 

5. Kitambulisho cha Mzanzibari Maombi yote yawasilishwe katika anuani ifuatayo; 

 

MKEMIA MKUU, 

WAKALA WA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI ZANZIBAR S.L.P 759, 

MARUHUBI ZANZIBAR.

 

BOFYA HAPA KUPATA PDF FILE YA TANGAZO HILI



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English