Nafasi za Kazi Ofisi ya Tume ya Mipango Pemba
Maelezo
Chanzo: Utumishi Zanzibar
Tarehe Iliyotolewa: 2020-08-31
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Ofisi ya Tume ya Mipango Pemba kama ifuatavyo:-
1. Afisa Mipango ya Watenda kazi Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Ustawi wa Jamii au Utawala wa Umma au ‘ Gender Issues’ au ‘Democrafy’ au ‘Planning’ Rasilimali Watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
2. Afisa Ufuatiliaji na Tathmini Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uchumi au Mipango kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
3. Afisa Mipango MKUZA Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mipango au Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
4. Mwanasheria Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
5. Tarishi Daraja la III “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amemaliza elimu ya Sekondari.
6. Dereva Daraja la III “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Mafunzo ya Udereva
• Awe na Leseni ya Udereva ilitolewa Zanzibar.
7. Afisa Ghala Msaidizi Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Ununuzi na Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
8. Afisa Mahusiano Daraja la II “Nafasi 1” – Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Mass Communication’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
9. Afisa Utumishi Msaidizi Daraja la III “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utawala wa Umma au Rasilimali Watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.
• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 04 Septemba, 2020 wakati wa saa za kazi