Nafasi za Kazi Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Matukio Zanzibar

Maelezo

Chanzo:

Tarehe Iliyotolewa: 2018-10-08

Download

Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 20306 ... Deadline: 2018-10-12 15:30:00

NAFASI ZA KAZI KATIKA OFISI YA WAKALA WA USAJILI WA MATUKIO YA KIJAMII ZANZIBAR

Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar inatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:-

1. AFISA TEHAMA (Nafasi 4 Makao Makuu, Unguja)

Sifa za Waombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe na elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya TEHAMA/Sayansi ya Komputa/Uhandisi wa Komputa/Mitandao ya Komputa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kipaumbele kitatolewa kwa wenye vyeti vya utaalamu kama CCNA, CCNP, MCSE, MCP, CISSP, JAVA,ORACLE, RED HAT na vyenginezo.
  • Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
  • Awe na uwezo wa kufanyakazi katika mazingira yenye shindikizo (Be able to work under pressure.)
  • Awe mpole kwa wateja

2. AFISA USAJILI WA WILAYA (Nafasi 11)

Sifa za Waombaji:

  • Awe Mzanzibari
  • Awe na elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya TEHAMA/Sheria/Uongozi wa Umma kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe amewahi kufanyakazi zaidi ya miaka 5 katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
  • Awe na uwezo wa kuongoza watu.
  • Awe na uwezo wa kufanyakazi katika mazingira yenye shindikizo (Be able to work under pressure.)
  • Awe mpole kwa wateja
  • Nafasi 7 Unguja na nafasi 4 Pemba.
  • Muombaji ainishe wilaya anayotaka kufanyia kazi katika ombi lake

3. MSAIDIZI AFISA TEHAMA (Nafasi 11)

Sifa za Waombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe na elimu ya Stashahada (Diploma) katika fani ya TEHAMA/Sayansi ya Komputa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kipaumbele kitatolewa kwa wenye vyeti vya utaalamu kama CCNA, CCNP, MCSE, MCP, A+, CISSP, JAVA,ORACLE, RED HAT na vyenginevyo.
  • Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
  • Awe na uwezo wa kufanyakazi katika mazingira yenye shindikizo (Be able to work under pressure.)
  • Awe mpole kwa wateja
  • Nafasi 7 Unguja na nafasi 4 Pemba.
  • Muombaji ainishe wilaya anayotaka kufanyia kazi katika ombi lake

4. MSAIDIZI AFISA USAJILI (Nafasi 9)

Sifa za Waombaji:

  • Awe Mzanzibari
  • Awe na elimu ya Stashahada/Cheti katika fani ya Utunzaji wa taarifa (Record management) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
  • Awe na uwezo wa kufanyakazi katika mazingira yenye shindikizo (Be able to work under pressure.)
  • Awe mpole kwa wateja
  • Nafasi 3 Makao Makuu, Nafasi 6 (Wilaya za Magharibi A, Magharibi B na Mjini)
  • Muombaji ainishe pahala anapotaka kufanyia kazi katika ombi lake

5. AFISA NDOA/TALAKA (Nafasi 1 Makao Makuu, Unguja)

 Sifa za Waombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe na elimu ya Shahada ya kwanza katika fani ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
  • Awe na uwezo wa kufanyakazi katika mazingira yenye shindikizo (Be able to work under pressure.)
  • Awe mpole kwa wateja

6. KARANI MUINGIZAJI TAARIFA (DATA ENTRY CLERK) (Nafasi 6 Makao Makuu)

Sifa za Waombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe na elimu ya Stashahada/Cheti katika fani ya TEHAMA kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
  • Awe na uwezo wa kufanyakazi katika mazingira yenye shindikizo (Be able to work under pressure.)
  • Awe mpole kwa wateja

7. KARANI WA KAUNTA (Nafasi 4, Makao Makuu)

Sifa za Waombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe na elimu ya Cheti cha Form IV cha NECTA
  • Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kiswahili.
  • Awe na uwezo wa kufanyakazi katika mazingira yenye shindikizo (Be able to work under pressure.)
  • Awe mpole kwa wateja

8. MASJALA (Nafasi 1, Makao Makuu)

Sifa za Waombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe na elimu ya Stashahada/Cheti katika fani ya Utunzaji wa Taarifa (Record Management) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kiswahili.
  • Awe na uwezo wa kufanyakazi katika mazingira yenye shindikizo (Be able to work under pressure.)
  • Awe mpole kwa wateja

JINSI YA KUOMBA:
Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

  • MKURUGENZI MTENDAJI,
    WAKALA WA USAJILI WA MATUKIO YA KIJAMII  ZANZIBAR,

            S. L. P 264
            ZANZIBAR

Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar iliyopo Jengo la Wizara ya Nchi,  Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mazizini Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii yaliopo katika jengo la Ofisi za Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali, Wete  Pemba. Muombaji anatakiwa kuiainisha nafasi ya kazi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Wale wote walioomba nafasi hizi kabla kwa kupitia Tume ya Utumishi Serikali wanaombwa wafanye maombi mapya moja kwa moja kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.

f) CV
g) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa. Muombaji anatakiwa aliwasilishe ombi lake MWENYEWE .
h) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 12 Oktoba, 2018 wakati wa saa za kazi.

Download

Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English