Kituo cha Kazi/Tukio: UngujaImetembelewa mara! 1764 ... Deadline: 2025-08-30 15:30:00
POST DETAILS
POST
AFISA UFATILIAJI UBORA WA DAWA SOKONI DARAJA LA II-UNGUJA - 1 POST
EMPLOYER
ZANZIBAR FOOD AND DRUG AGENCY (ZFDA)
APPLICATION TIMELINE:
From: 16-08-2025 To: 30-08-2025
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
Majukumu:
Kushiriki katika utekelezaji wa shughuli za Ufuatiliaji wa Bidhaa Sokoni (PMS).
Kufuatilia na kutathmini usalama na ufanisi wa bidhaa za dawa zilizoko sokoni.
Kushiriki katika uchambuzi wa data kutoka kwa tafiti za ufuatiliaji wa moja kwa moja.
Kuchunguza matukio mabaya makubwa yanayotokana na matumizi ya Chanjo (AEFI) na matukio yanayokidhi vigezo vya uchunguzi;
Kujibu ripoti na malalamiko yanayohusiana na bidhaa zenye ubora duni;
Kuwasiliana na kutoa maoni kwa wadau kuhusu shughuli za PMS;
Kushiriki katika utayarishaji wa Miongozo na Taratibu Sanifu za Kiutendaji (SOPs).
Kuandaa ripoti za utekelezaji wa viashiria (indicators) vya WHO Global Benchmarking Tools (GBT);
Kutoa msaada wa kitaalamu ili kuboresha mifumo ya udhibiti na kuhakikisha inalingana na matakwa ya WHO Maturity Level 3
Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada kwanza au Shahada ya pili ya Ufamasia kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Awe na uelewa wa viwango vya WHO GBT (Global Benchmarking Tool),
Awe na uzoefu wa kusimamia mpango wa uwiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kufikia kiwango cha Ukamilifu cha Shirika la Afya Duniani (WHO Maturity Level 3)