Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Daraja la II-PEMBA - 1 POST

Maelezo

Chanzo: zan ajira



Tarehe Iliyotolewa: 2025-08-16



Kituo cha Kazi/Tukio: PEMBA
Imetembelewa mara! 518 ... Deadline: 2025-08-30 15:30:00

POST DETAILS

POSTAfisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Daraja la II-PEMBA - 1 POST
EMPLOYERZANZIBAR FOOD AND DRUG AGENCY (ZFDA)
APPLICATION TIMELINE:From: 16-08-2025 To: 30-08-2025
DUTIES AND RESPONSIBILITIES

Majukumu:

  1. Kusaidia katika usanidi, usasishaji na uendeshaji wa mifumo ya kompyuta ya ZFDA;
  2. Kufuatilia utendaji wa mifumo na kuripoti matatizo kwa ngazi ya juu;
  3. Kutoa msaada kwa watumiaji kuhusu matumizi ya mifumo ya kiutawala na kiufundi;
  4. Kusaidia katika kuweka hatua za usalama wa mifumo ya TEHAMA;
  5. Kufanya matengenezo ya kawaida (routine maintenance) ya mifumo;
  6. Kutunza kumbukumbu sahihi za usanidi na mabadiliko ya mfumo;
  7. Kusaidia katika utekelezaji wa sera na taratibu za TEHAMA;
  8. Kushiriki katika mafunzo na kuboresha ujuzi kuhusu mifumo mbalimbali ya taasisi;
  9. Kusaidia katika kusimamia tovuti za taasisi;
  10. Kutunza nyaraka za mifumo ya TEHAMA na taratibu zake;
  11. Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo mwaka, nusu mwaka na mwaka.
  12. Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE

Sifa za Muombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘TEHAMA kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na uzoefu wa kusimamia na kutumia mifumo ya kielektroniki pamoja na miradi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inayohusiana na mifumo.
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.
REMUNERATIONZPSH-10



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2025 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English