Nafasi za Kazi Tasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar
Maelezo
TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO ZANZIBAR
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
BODI YA WAKURUGENZI YA TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO ZANZIBAR KWA MUJIBU WA SHERIA INATANGAZA NAFASI ZA KAZI KATIKA OFISI ZAKE UNGUJA NA PEMBA KWA WATAFITI KATIKA KADA MBALIMBALI KAMA IFUATAVYO.
1. AFISA UTAFITI KILIMO DARAJA LA II - UNGUJA NAFASI 2 NA PEMBA NAFASI 5
Sifa za Muombaji
Awe Mzanzibari
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza au Shahada ya Pili katika fani ya ‘General Agriculture’ au fani inayolingana na hiyo katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Awe na umri usiozidi miaka 46.
2. AFISA UTAFITI UMWAGILIAJI MAJI DARAJA LA II - UNGUJA NAFASI 1
Sifa za Muombaji
Awe Mzanzibari
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza au Shahada ya Pili katika fani ya ‘Water Resources and Irrigation Engineering’ au fani inayolingana na hiyo katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Awe na umri usiozidi miaka 46.
3. AFISA MAABARA DARAJA LA II - UNGUJA NAFASI 3
Sifa za Muombaji
Awe Mzanzibari
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza au Shahada ya Pili katika fani ya ‘Laboratory Science au Biotechnology au Molecular Biology au Microbiology’ au fani inayolingana na hizo katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Awe na umri usiozidi miaka 46
TAFADHALI PAKUA PDF FILE HAPA KWA TAARIFA ZAIDI