Nafasi za Kazi Wizara ya Afya
Maelezo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb.Na.JA.9/259/01/A/79 5 Mei, 2022 TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi kumi na tisa (19) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.
1.0 MWAJIRI: KATIBU MKUU, WIZARA YA AFYA
1.0.1 AFISA USTAWI WA JAMII DARAJA LA II - (NAFASI 15)
1.0.2 MAJUKUMU YA KAZI
- Kuendesha Usaili wa wahudumiwa (watu wenye ulemavu, wazee, familia zenye matatizo, watoto na vijana wenye matatizo mbalimbali);
- Kufanya ukaguzi wa mazingira wanayoishi wahudumiwa ili kupata taarifa zao kamili;
- Kuandaa taarifa za usaili na ukaguzi wa mazingira ya wahudumiwa;
- Kupokea na kukusanya taarifa za Ustawi wa Jamii kutoka kwa wadau na vituo mbalimbali vya Ustawi wa Jamii;
- Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu huduma za watu wenye ulemavu, wazee, malezi ya watoto na familia zenye matatizo;
- Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya uandikishaji vituo vya kulelea watoto wadogo mchana, malezi ya kambo (foster care) na vituo vya walezi wa watoto wadogo mchana;
- Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya msaada wa Rais kutoka kwa akina mama, waliojifungua watoto watatu au zaidi kwa mara moja;
- Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya watoto yatima au wanaohitaji misaada mbalimbali;
- Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali toka kwenye familia za watu wenye dhiki;