Nafasi za Kazi Wizara ya Afya Zanzibar
Maelezo
Chanzo: Utumishi Zanzibar
Tarehe Iliyotolewa: 2022-07-30
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Afya Zanzibar kwa ajili ya Hospitali kuu, Hospitali ya Mkoa na Hospitali za Wilaya Unguja na Pemba Kama ifuatavyo:-
1. DAKTARI WA BINAADAM DARAJA LA II (ZPSJ-09) Nafasi 155, Unguja 120 na Pemba 35
Sifa za waombaji
? Awe mwenye Shahada ya kwanza katika fani ya Tiba ya Binaadamu (Medical Doctor) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
? Awe amemaliza mafunzo ya vitendo (Internship) kwa muda wa mwaka mmoja katika hospitali zilizoteuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
? Awe amesajiliwa na Baraza la Madaktari Zanzibar.
Majukumu
i. Kufanya shughuli zote za utibabu, huduma za upasuaji wa dharura na upasuaji wa kawaida.
ii. Kusimamia wafanyakazi walio chini yake.
iii. Kuchunguza, kufatilia na kuzuia miripuko ya magonjwa mbali mbali.
iv. Kupanga na Kufanya tathmini ya huduma za afya.
v. Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za afya
vi. Kutoa huduma za “Outreach Programme”.
2. DAKTARI WA MENO DARAJA LA II (ZPSJ-09) Nafasi 17, Unguja nafasi 10 na Pemba nafasi 7.
Sifa za waombaji
? Awe mwenye Shahada ya kwanza katika fani ya Tiba ya Meno (Dental surgery) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
? Awe amemaliza mafunzo ya vitendo (Internship) kwa muda wa mwaka mmoja katika hospitali zilizoteuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
? Awe amesajiliwa na Baraza la Madaktari Zanzibar.
Majukumu
i. Kufanya shughuli zote za utibabu na upasuaji wa kawaida wa kinywa na meno.
ii. Kutoa ushauri nasaha na kusimamia elimu ya afya ya kinywa na meno.
iii. Kusimamia wafanyakazi walio chini yake.
iv. Kuchunguza, kufatilia na kuzuia magonjwa ya kinywa na meno
v. Kuweka meno bandia.
vi. Kufundisha wanafunzi na watumishi waliopo kwenye eneo lake la kazi.
vii. Kufanya utafiti wa maradhi ya kinywa na meno na kutoa matokeo.
viii. Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma ya Afya ya kinywa na meno.
ix. Kutoa huduma za “outreach programme”.
x. Kufanya tathmini ya huduma ya matibabu ya meno.
xi. Kutunza takwimu na kuzitumia.
3. AFISA MAABARA DARAJA II (ZPSG-09) Nafasi 15, Unguja nafasi 5 na Pemba nafasi 10
Sifa za waombaji
? Awe wenye Shahada ya kwanza katika fani ya Maabara za Afya (Medical Laboratory Scientist) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
? Awe amemaliza mafunzo ya vitendo (internship)
? Awe kusajiliwa na Bodi ya Wataalamu wa Maabara ya Afya.
Majukumu
i. Kukagua na kuchukuwa sampuli zinazo hitaji utaalamu maaalum au uchunguzi maaalum wa ziada katika maabara nyengine za Afya na utafiti.
ii. Kutunza kumbukumbu na vifaa vya maabara
iii. Kusaidia Kutoa ushauri, kufanya au kushiriki tafiti tofauti.
iv. Kusaidia kutunza vifaa na vitendanishi vya maabara.
v. Kuwasimamia wafanyakazi waliochini yake katika utendaji wao wa kazi za kila siku pamoja na mafundi (Biomedical Engineering)
vi. Kufundisha wanafunzi katika tasisi mbalimbali za Afya, kwa masomo yanayoendana na taaluma ya maabara
vii. Kutoa ushauri kwa maeneo yanayomuhusu
4. AFISA MIONZI (MEDICAL RADIOGRAPHER) DARAJA LA II (ZPSG-09) Nafasi 7, Unguja 4 na Pemba 3
Sifa za waombaji
? Awe mwenye Shahada ya kwanza katika fani ya Mionzi (Medical Radiographer) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Majukumu
i. Kutoa huduma za Mionzi.
ii. Kusaidia kufundisha wafanyakazi na wafanyakazi mambo yote yahusianayo na ultrasound
iii. Kushiriki katika kutathmini usalama wa wagonjwa kutokana na mashine za ultrasound.
iv. Kushiriki katika kufanya utafiti zifanyazo katika sehemu yake.
5. MFIZIOTHERAPIA DARAJA LA II (ZPSG-09) Nafasi 5 Pemba
Sifa za waombaji
? Awe mwenye Shahada ya kwanza Fiziotherapia kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Majukumu
i. Kutibu wagonjwa kwa kutumia umeme.
ii. Kuwafanyisha mazoezi wagonjwa wa viungo
iii. Kuandaa bajeti ya mahitaji ya sehemu ya kazi za viungo.
iv. Kutoa ushauri utakaowezesha kuimarisha huduma za maradhi ya viungo.
6. AFISA AFYA MAZINGIRA DARAJA LA II (ZPSG-09)Nafasi 19, Unguja nafasi 14 na Pemba nafasi 5
Sifa za waombaji
? Awe mwenye Shahada ya kwanza ya Afya Jamii au Afya na Mazingira katika kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
? Awe amemaliza mafunzo ya vitendo (internship)
Majukumu
i. Kutambua mambo ya kiafya na mazingira katika jamii
ii. Kukusanya, kuzihifadhi, kuzichambua na kuzifanyia kazi taarifa za Afya na mazingira katika jamii.
iii. Kufanya tathmini juu ya uhitaji wa huduma za Afya na mazingira katika jamii
iv. Kutekeleza viwango (sanitation and hygiene standard) katika jamii
v. Kuhamasisha jamii juu ya usalama wa chakula na maji
vi. Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maeneo mbali mbali ya kijamii
vii. Kudhibiti wadudu na wanyama waharibifu wenye kuleta maambukizi ya magonjwa katika jamii.
viii. Kuchunguza ramani za ujenzi kabla na baada ya ujenzi ili kudhibiti makaazi yasiozingatia kanuni za Afya na mazingira katika jamii
ix. Kutoa hati ruhusa ya kuishi baada ya nyumba kumalizika kujengwa
x. Kufanya ukaguzi wa mahoteli, nyumba za kulala wageni na biashara
xi. Kutekeleza sheria zinazohusu Afya ya jamiina mazingira
xii. Kuwaelekeza kazi maafisa wa Afya walio chini yake
xiii. Kuelimisha jamii juu ya mbinu za kujikinga na kupambana na mlipuko ya magonjwa
xiv. Kutoa elimu ya Afya kwa jamii
7. MFAMASIA DARAJA LA II (ZPSG-09)Nafasi 13; Unguja nafasi 10 na Pemba nafasi 3
Sifa za waombaji
? Awe mwenye Shahada ya Kwanza ya Ufamasia kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
? Awe amemaliza mafunzo ya mazoezi ya vitendo (internship) ya muda wa mwaka mmoja (1).
? Awe amesajiliwa na Bodi ya Vyakula na Dawa Zanzibar.
Majukumu
i. Kuainisha na kutayarisha mahitaji ya mwaka ya dawa na vifaa vyengine vya kitabibu.
ii. Kutayarisha bajeti kwa ajili ya dawa na vifa vya kitabibu.
iii. Kufanya manunuzi, kuhifadhi na kuhakiki dawa.
iv. Kusimamia na kushauri matumizi bora ya dawa.
v. Kugawa dawa na vifaa vya kitabibu kwa wagonjwa.
vi. Kutengeneza na kuchanganya dawa.
vii. Kuandika ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.
8. AFISA USHAURI NASAHA DARAJA LA II (ZPSG-09)Nafasi 18; Unguja nafasi 14 na Pemba nafasi 4
Sifa za waombaji
Awe mwenye Shahada ya Kwanza ya Ushauri Nasaha/Ustawi wa Jamii kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Majukumu
i. Kushiriki katika kusikiliza malalamiko yanayohusu ukiukwaji wa haki na maendeleo ya wanawake.
ii. Kushiriki katika kuhamasisha jamii juu ya kujihusisha katika masuala mbalimbali yatakayoleta ustawi mwema wa maendeleo ya jamii.
iii. Kusaidia kuelimisha Jamii kuepukana na mila potofu zinazokwenda kinyume na mila na desturi za Jamii.
iv. Kusaidia kutoa ushauri nasaha kwa watu wenye matatizo mbali mbali katika jamii.
v. Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.
9. MUUGUZI DARAJA LA II (ZPSG-09)nafasi 165; Unguja nafasi 120 na Pemba nafasi 45
Sifa za waombaji
? Awe mwenye Shahada ya kwanza katika fani ya uuguzi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
? Awe amemaliza mafunzo ya vitendo (internship)
? Awe amesajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar.
Majukumu
i. Kutumia utaratibu wa kubainisha mifumo ya Uuguzi na Ukunga (Nursing Process).
ii. Kutunza vifaa vya kazi.
iii. Kufanya kazi za kiuguzi za kuhudumia wateja katika jamii, hospitali na sehemu zote zinapotolewa huduma za Afya.
iv. Kukusanya takwimu muhimu za Afya.
v. Kuwaelekeza na kusimamia wauguzi na wakunga walio chini yake.
vi. Kutayarisha mpango wa kazi kwa ajili ya huduma za uuguzi na Ukunga.
vii. Kutoa huduma za kinga na uzazi
viii. Kuelimisha wagonjwa na jamii
10. TABIBU (CLINICAL OFFICER) DARAJA LA III (ZPSF-01) nafasi 40; Unguja nafasi 20 na Pemba nafasi 20
Sifa za waombaji
? Awe mwenye elimu ya Stashahada ya utabibu (Clinical Medicine) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
? Awe na leseni ya Tabibu Kutoka Baraza la Madaktari Zanzibar.
Majukumu
i. Kuchambua na kupanga na kutekeleza huduma za afya ya msingi
ii. Kutambua na kutibu mgonjwa wa kawaida
iii. Kuweka kumbukumbu za vifaa na zana za kutolea huduma.
11. TABIBU WA MENO (DENTAL THERAPIST) DARAJA LA III (ZPSF-01)Nafasi 34; Unguja nafasi 21 na Pemba nafasi 13
Sifa za waombaji.
? Awe mwenye Stashahada ya Tabibu Meno kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali
? Awe na leseni ya Utabibu meno kutoka Baraza la Madaktari Zanzibar.
Majukumu
i. Kuchambua na kupanga na kutekeleza huduma za Afya ya msingi ya Kinywa na Meno.
ii. Kutoa huduma ya kwanza kwa matatizo yatokanayo na ajali
iii. Kutambua na kutibu mgonjwa wa kawaida wa kinywa na Meno
iv. Kuweka kumbukumbu za vifaa na zana za kutolea huduma.
v. Kutoa huduma ya Kinga na Tiba ya meno.
vi. Kutoa Elimu ya Afya ya kinywa (Oral Health) skuli na kwa jamii
vii. Kuweka kumbukumbu za wagonjwa na kuandaa taarifa za utekelezaji.
viii. Kung’owa meno ya kawaida na kufanya upasuaji mdogo.
ix. Kufanya tathmini ya huduma za Afya ya Kinywa na Meno.
12. MUUGUZI MSAIDIZI DARAJA LA III (ZPSF-01) Nafasi 195; Unguja nafasi 135 na Pemba nafasi 60
Sifa za waombaji.
? Awe mwenye Stashahada ya kawaida katika fani ya Uuguzi na Ukunga (Nursing and Midwifery) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
? Awe amesajiliwa na Baraza la Wauguzi na Ukunga.
Majukumu
i. Kutoa huduma za kinga na uzazi.
ii. Kutambua matatizo ya wagonjwa
iii. Kutoa huduma kwa wangonjwa majumbani.
iv. Kutoa huduma za uuguzi na ukunga kwa wagonjwa.
v. Kufanya uchunguzi sahihi wa hali ya Afya ya mgonjwa ili kumsaidia.
vi. Kukusanya taarifa muhimu kutoka kwa mgonjwa kuhusu Afya yake.
vii. Kusimamia usafishaji wa vyombo vya tiba (Sterilization).
viii. Kutayarisha mpango wa huduma za mgonjwa (Nursing Care Plans) na kuzitekeleza.
ix. Kutathmini maendeleo ya mgonjwa na kutoa taarifa kwa daktari.
13. AFISA MAABARA MSAIDIZI DARAJA LA III (ZPSF-01) Nafasi 15 Pemba
Sifa za waombaji.
Awe mwenye Stashahada ya kawaida katika fani Maabara (Medical laboratory Technician) kutoka Katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Majukumu
i. Kupima sampuli za maradhi mbali mbali.
ii. Kutengeneza dawa za kufanyia vipimo vya maabara.
iii. Kuchukua sampuli za wagonjwa wanaohitaji huduma za maabara
iv. Kuhifadhi sampuli mbali mbali zinazotakiwa kufanyiwa uchunguzi.
v. Kufanya kazi za ukaguzi wa maabara, vitendanishi, vifaa, kemikali na hifadhi ya kemikali
vi. Kuweka kumbukumbu za maabara ambazo zimepatikana wakati wa uchunguzi.
14. MFIZIOTHERAPIA MSAIDIZI DARAJA LA III (ZPSF-01) Nafasi 14; Unguja nafasi 12 na Pemba nafasi 2
Sifa za waombaji
Awe mwenye Shahada ya kwanza ya fiziotherapia kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Majukumu
i. Kufanya kazi za kupokea na kuwaandaa wagonjwa katika maeneo ya tiba ya Fiziotherapia.
ii. Kuandaa chumba kwa ajili tiba ya mgonjwa
iii. Kuandaa kumbukumbu za mgonjwa kabla ya matibabu
iv. Kutoa usaidizi wa tiba kwa vitendo kwa maelekezo ya Fiziotherapisti kama vile kuchezesha viungo, kufundisha mwendo
v. Kutoa tiba za vitendo kwa kufuata mpango wa matibabu wa mfiziotherapia kwa mgonjwa
vi. Kutoa usimamizi kwa wagonjwa wanaondelea na tiba za vitendo kama vile mazoezi ya viungo
vii. Kutunza kumbukumbu zinazohusiana matibabu vitendo yaliyotolewa na matokeo yake
15. BIBI/BWANA AFYA (HEALTH ASSISTANT) DARAJA LA III (ZPSF-01) Nafasi 25; Unguja nafasi 12 na Pemba nafasi 13
Sifa za waombaji.
Awe mwenye Stashahada ya Kawaida (Ordinary Diploma) katika fani ya Afya ya Mazingira/Afya ya jamii (Community Health/Enviromental Health) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Majukumu
i. Kudhibiti na kuzuia maradhi ya miripuko na kutoa chanjo kwa wasafiri.
ii. Kudhibiti wadudu na wanyama wanaoeneza magonjwa ya kuambukiza.
iii. Kuelimisha jamii kuhusu Afya ya Mazingira.
iv. Kusimamia ukaguzi wa maji na vyakula na kuchukua sampuli kwa ajili ya ukaguzi.
v. Kupendekeza maeneo ya ujenzi kwa kushirikiana na sekta nyengine za kijamii.
vi. Kusimamia mazishi ya maiti wa maradhi ya kuambukiza.
vii. Kuandaa taarifa za ukaguzi wa Mazingira.
viii. Kuandika ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.
16. MFAMASIA MSAIDIZI DARAJA LA III (ZPSF-01)Nafasi 70; Unguja nafasi 45 na Pemba nafasi 25
Sifa za waombaji.
Awe mwenye Stashahada ya Kawaida (Ordinary Diploma) ya Uchanganyaji Madawa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Majukumu
i. Kuchanganya na kutayarisha Dawa kwa ajili ya wagonjwa.
ii. Kutoa maelekezo ya matumizi bora ya dawa.
iii. Kugawa dawa kwa mujibu wa maelekezo ya Daktari.
iv. Kuhifadhi dawa muhimu zilizosalia.
v. Kutunza kumbukumbu za ugawaji na matumizi ya dawa.
vi. Kutayarisha makisio ya madawa yanayohitajika na vifaa vya matibabu.
vii. Kuwaelekeza Watumishi walioko chini yake.
viii. Kutoa ushauri wa matumizi sahihi ya dawa.
ix. Kuandaa taarifa ya ugawaji wa dawa muda baada ya muda.
x. Kuandika ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.
17. AFISA MSAIDIZI USHAURI NASAHA DARAJA LA III (ZPSF-01) Nafasi 8 Unguja
Sifa za waombaji.
Awe mwenye Stashahada ya Ushauri Nasaha, Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Jamii au fani inayolingana nazo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Majukumu
i. Kushiriki katika kusikiliza malalamiko yanayohusu ukiukwaji wa haki na maendeleo ya wanawake.
ii. Kushiriki katika kuhamasisha jamii juu ya kujihusisha katika masuala mbalimbali yatakayoleta ustawi mwema wa maendeleo ya jamii.
iii. Kusaidia kuelimisha Jamii kuepukana na mila potofu zinazokwenda kinyume na mila na desturi za Jamii.
iv. Kusaidia kutoa ushauri nasaha kwa watu wenye matatizo mbali mbali katika jamii.
v. Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.
JINSI YA KUOMBA:
• Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa Kielektronic wa ajira (Zanajira) kupitia anuani ifuatayo:- http://portal.zanajira.go.tz kuanzia tarehe 01 Agosti, 2022 hadi tarehe 21 Agosti, 2022
• Mfumo huo pia unapatikana katika tovuti ya Tume ya Utumishi Serikalini www.zanajira.go.tz
• Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi ya kazi pamojana Wilaya anayoiombea.
Kwa msaada wa kitaalamu wasiliana na Tume ya Utumishi Serikalini kupitia email zifuatazo:-
1. info@zanajira.go.tz
2. habari@zanajira.go.tz
3. maulizo@zanajira.go.tz
TANBIHI:
Tume ya Utumishi Serikalini inawatahadharisha waombaji wote kwamba ajira zinatolewa bure. Hivyo, wanatakiwa kujiepusha na Matapeli wanaotumia nafasi hizi kwa kujipatia kipato kisicho cha halali.