Nafasi za Kazi Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Zanzibar

Maelezo

Chanzo: Utumishi Zanzibar



Tarehe Iliyotolewa: 2018-08-20



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 16811 ... Deadline: 2018-08-24 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Wizara ya Ardhi, Nyumba Maji na Nishati Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-

1. Mtunza Ghala Daraja la III “Nafasi 1” – Unguja na “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na elimu ya Stashahada katika fani ya ‘Material Management’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

2. Afisa Uhusiano Daraja la II “Nafasi 1” Pemba 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Uhusiano wa Umma (Public Relation) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Afisa Tehama Daraja la II “Nafasi 1” Pemba 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Computer Engineering kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Afisa Geo Informatic System (GIS) Daraja la II “Nafasi 3” Unguja na “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Geo Informatic System “GIS” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Mpima Ardhi Daraja la II “Nafasi 1” Pemba 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya “Surveying” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar






6. L.R.MGT Daraja la II “Nafasi 3” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na elimu ya Shahada ya Kwanza ya “Land Management” au “Estate Management” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

7. Urban Planning Daraja la II “Nafasi 2” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya “Urban and Rural Planning” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

8. Land Lease Daraja la III “Nafasi 2” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya “Land Management and Valuation” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

9. Valuer Daraja la II “Nafasi 4” Unguja na “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya “Land Management and Valuation” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

10. Land Ranger Daraja la III “Nafasi 2” Unguja na “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya “Civil Engineering” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

11. Afisa Shamba Daraja la II “Nafasi 1” Pemba 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Kilimo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

12. Msaidizi Urban Planning Daraja la III “Nafasi 1” Pemba 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya “Urban and Rural Planning” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

13. Taarishi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na elimu ya Sekondari na kufaulu.

MAHKAMA YA ARDHI:
14. Mlinzi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na elimu ya Sekondari na kupata Mafunzo ya Ulinzi JKU au JKT.

15. Katibu Muhtasi Daraja la III “Nafasi 2” Unguja na “Nafasi 1” Pemba 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Ukatibu Muhtasi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

AFISI YA MTATHMINI WA SERIKALI:
16. Afisa Tathmini Daraja la II “Nafasi 3” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya “Land Management and Valuation” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

17. Afisa Sheria Daraja la II “Nafasi 1” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

18. Afisa Uchumi Daraja la II “Nafasi 2” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar



19. Mtunza Kumbukumbu Daraja la III “Nafasi 1” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

20. Dereva Daraja la III “Nafasi 1” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amemaliza elimu ya Sekondari na kupata Mafunzo ya Udereva
• Awe na Leseni ya Udereva.

21. Afisa Manunuzi Daraja la II “Nafasi 1” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Ununuzi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

22. Afisa Tehama Daraja la II “Nafasi 1” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Computer Science kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

23. Taarishi Daraja la III “Nafasi 1” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na elimu ya Sekondari na kufaulu.

24. Mtunza Ghala Daraja la III “Nafasi 1” – Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na elimu ya Stashahada katika fani ya ‘Material Management’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI, S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuiainisha nafasi ya kazi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa. Muombaji anatakiwa aliwasilishe ombi lake MWENYEWE .
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 24 Agosti, 2018 wakati wa saa za kazi.
 



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English