Nafasi za Kazi Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Zanzibar

Maelezo

Chanzo: Utumishi Zanzibar



Tarehe Iliyotolewa: 2020-07-24



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 37994 ... Deadline: 2020-07-30 15:30:00

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WIZARA YA ARDHI, NYUMBA, MAJI NA NISHATI ZANZIBAR

Posted: 2020-07-24 14:19:32

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-

1. Katibu Mukhtasi Daraja la III “Nafasi 3” Unguja

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.

• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Uhazili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Afisa kumbukumbu Daraja la II “Nafasi 1” Unguja

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.

• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Utunzaji Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Mwangalizi wa Ofisi Daraja la III “Nafasi 2” Unguja

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.

• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utawala wa Umma au Rasilimali Watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Afisa Utumishi Daraja la II “Nafasi 1” Unguja

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.

• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Utawala wa Umma au Rasilimali Watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Afisa Sheria Daraja la II “Nafasi 2” Unguja na “Nafasi 1” Pemba

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.

• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6. Karani Mapokezi Daraja la III “Nafasi 1” Unguja

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.

• Awe amehitimu Cheti katika fani ya Mapokezi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

7. Afisa Sera Daraja la II “Nafasi 1” Unguja

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.

• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uchumi au Mipango kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

8. Muhudumu Daraja la III “Nafasi 3” Unguja

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.

• Awe amemaliza elimu ya Sekondari.

9. Fundi Seremala Daraja la III “Nafasi 1” Unguja

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.

• Awe amehitimu Cheti katika fani ya Ufundi Seremala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

10. Fundi Sanifu Ujenzi Daraja la III “Nafasi 1” Unguja

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.

• Awe amehitimu elimu ya cheti katika fani ya Ujenzi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

11. Ulinzi Daraja la III “Nafasi 3” Unguja

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.

• Awe amemaliza elimu ya Sekondari na kupata Mafunzo ya Ulinzi (JKU) au (JKT).

12. Technician Daraja la III “Nafasi 1” Unguja

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.

• Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya “Civil Engineer” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

13. Msaidizi Mpimaji Daraja la III “Nafasi 1” Unguja

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.

• Awe amemaliza elimu ya Sekondari

14. Karani Mahkama Daraja la III “Nafasi 2” Unguja

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.

• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

15. Dereva Daraja la III “Nafasi 1” Unguja

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.

• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Mafunzo ya Udereva

• Awe na Leseni ya Udereva ilitolewa Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:

• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU,

TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,

S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-

a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo

b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)

c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.

d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.

e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.

f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.

g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 30 Julai, 2020 wakati wa saa za kazi



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English