Nafasi za Kazi Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar
Maelezo
Chanzo: Utumishi Zanzibar
Tarehe Iliyotolewa: 2018-08-11
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Wizara ya Fedha na Mipango – Pemba kama ifuatavyo:-
1.Afisa Uchumi Daraja la II “Nafasi 2” - Pemba
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Uchumi’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
1.Afisa Kodi Daraja la II “Nafasi 3” - Pemba
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza katika fani ya Usimamizi wa Kodi ‘Taxation Management’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.
•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuiainisha nafasi ya kazi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa. Muombaji anatakiwa aliwasilishe ombi lake MWENYEWE .
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 17 Agosti, 2018 wakati wa saa za kazi.
•Tangazo hili pia linapatikana katika Tovuti WWW.LPS.GO.TZ