Nafasi za Kazi Wizara ya Maji
Maelezo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Ref.No.JA.9/259/01/A/60
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu Wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi Wa Umma kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi kumi (10) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.
1.0 MWAJIRI: KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI 1.0.1 MHAIDROJIA II (HYDROLOGIST II) NAFASI 6
1.0.2 MAJUKUMU YA KAZI
I. kusimamia ujenzi na usimamizi wa ukarabati wa vituo vya hali ya hewa, vituo vya upimaji uwingi wa maji kwenye mitoni mabwawa na maziwa (discharge measurements);
II. Uchukuaji wa sampuli za mchanga unaosafirishwa kwenye mito (sediment sampling) na kuzitafsiri;
III. kufanya uhakiki wa takwimu (validation activities) wakati wa kuchakata takwimu.
kuratibu ukusanyaji wa takwimu/taarifa zote za kihaidrolojia kutoka madakio na vidakio vya maji (catchments/sub catchments) na kuhakikisha takwimu zote kutoka kila kituo zinatumwa makao makuu ya bonde kila mwezi na tarehe 15 ya kila mwezi unaofuata zinawasilishwa wizarani;
Kufanya uchunguzi wa awali wa shughuli zinazohusu vituo vya haidrolojia;