Nafasi za Kazi Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Maelezo

Chanzo: Utumishi Zanzibar



Tarehe Iliyotolewa: 2018-07-06



Kituo cha Kazi/Tukio: Unguja
Imetembelewa mara! 25917 ... Deadline: 2018-07-11 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Unguja kama ifuatavyo:-

1. Afisa mipango Daraja la II “Nafasi 3” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mipango/Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

2. Afisa Utawala Daraja la II “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Utawala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

3. Afisa Michezo Daraja la II “Nafasi 3” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Utawala/ Rasilimali watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Afisa Uhusiano wa Kijamii Daraja la II “Nafasi 2” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mahusiano ya Umma (PRO) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Katibu wa Waziri Daraja la II “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani Utawala/ Rasilimali watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6. Msaidizi Mtunza ghala Daraja la III “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Manunuzi na Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.






7. Msaidizi Afisa Manunuzi Daraja la III “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Manunuzi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

8. Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 2” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

9. Afisa IT Msaidizi Daraja la III “Nafasi 2” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya IT kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

10. Katibu Muhtasi Daraja la III “Nafasi 3” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Ukatibu Muhtasi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

11. Wahudumu Daraja la III “Nafasi 3” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Form Sekondari.

12. Dereva Daraja la III “Nafasi 2” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Cheti cha Udereva na leseni hai class C kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

13. Walinzi Daraja la III “Nafasi 6” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari. 
• Awe amemaliza elimu ya Sekondari.
• Awe amepata mafunzo ya Ulinzi (Mgambo au JKU au JKT)

14. Taarishi Daraja la III “Nafasi 3” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari. 

15. Watunza Uwanja wa Amani Daraja la III “Nafasi 9” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari. 
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari.

16. Watunza Bustani Daraja la III “Nafasi 3” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari. 
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari.


Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 11 Julai, 2018 wakati wa saa za kazi.



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English