Nafasi za Kazi Za Ukutubi Wizara ya Elimu Zanzibar

Maelezo

Chanzo: Utumishi Zanzibar



Tarehe Iliyotolewa: 2018-05-17



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 17103 ... Deadline: 2018-05-23 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi 41 za kazi ya Ukutubi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-

NAM. IDARA IDADI YA NAFASI MAHALI
1 IDARA YA ELIMU YA SEKONDARI 32 UNGUJA
2 IDARA YA MAFUNZO YA UALIMU 5 UNGUJA
3 IDARA YA MAFUNZO YA UALIMU 4 PEMBA

Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Ukutubi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 23 Mei, 2018 wakati wa saa za kazi.



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English