Nafasi za Kazi Zanzibar State Trading Corporation (ZSTC)

Maelezo

Chanzo: ZSTC Web



Tarehe Iliyotolewa: 2020-06-24


Download


Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 38323 ... Deadline: 2020-06-29 15:30:00

SHIRIKA LA BIASHARA LA TAIFA ZANZIBAR (ZSTC) 

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI 

 

Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC) linatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo;- 

 

1. Dereva Daraja la III: Nafasi 2 Unguja, 1 Pemba 

 

Sifa za muombaji 

 

? Awe Mzanzibari 

? Asiwe muajiriwa wa Serikali. 

? Awe amemaliza elimu ya sekondari. 

? Awe na cheti cha kuhitimu mafunzo ya udereva kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). 

? Awe na leseni halali ya Udereva iliyohai ya Daraja B1 na C. 

? Awe na uzoefu wa udereva usiopungua miaka 3. 

 

2. Afisa Utumishi Daraja la II: Nafasi 1 Unguja 

 

Sifa za muombaji 

 

? Awe Mzanzibari 

? Asiwe muajiriwa wa Serikali. 

? Awe na elimu ya shahada ya kwanza katika fani ya Usimamizi wa Rasilimali watu (Human Resource Management), au Utawala (Public Administration), au fani inayoendana nayo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). 

? Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

 

3. Afisa Takwimu Daraja la II: Nafasi 1 Unguja 

 

Sifa za muombaji 

 

? Awe Mzanzibari. 

? Asiwe muajiriwa wa Serikali. 

? Awe na elimu ya Shahada ya kwanza ya Takwimu (Statistics) au fani nyengine inayoendana nayo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). 

? Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

 

4. Mtaalamu wa Kilimo Daraja la II/III (Agronomist): Nafasi 1 Unguja, 1 Pemba. 

 

Sifa za muombaji 

 

? Awe Mzanzibari 

? Asiwe muajiriwa wa Serikali. 

? Awe na elimu ya Stashahada au Shahada ya kwanza katika fani ya “Agronomist” au “General Agriculture”, au fani nyengine inayoendana nayo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). 

? Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

 

5. Afisa Masoko Daraja la II: Nafasi 2 Unguja 

 

Sifa za muombaji 

 

? Awe Mzanzibari 

? Asiwe muajiriwa wa Serikali. 

? Awe na elimu ya Shahada ya kwanza katika fani Masoko (Marketing) au fani nyengine inayoendana nayo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). 

? Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

 

6. Afisa Udhibiti wa Ubora wa Bidhaa Daraja la II: Nafasi 1 Unguja 

 

Sifa za muombaji 

 

? Awe Mzanzibari 

? Asiwe muajiriwa wa Serikali. 

? Awe na elimu ya Shahada ya kwanza katika fani ya “Food Science & Technology, au “Science in Human Nutrition”, au fani nyengine inayoendana nayo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). 

? Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

 

7. Mhandisi wa Umeme (Electrical Engineer) Daraja la II: Nafasi 1 Kiwanda cha Makonyo - Pemba 

 

Sifa za muombaji 

 

? Awe Mzanzibari. 

? Asiwe muajiriwa wa Serikali. 

? Awe na elimu ya Shahada ya kwanza katika fani ya Uhandisi Umeme (Electrical Engineer) au Mechatronics Engineer kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). 

? Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.  

 

8. Afisa Manunuzi Daraja la II: Nafasi 1 Pemba 

 

Sifa za muombaji 

 

? Awe Mzanzibari. 

? Asiwe muajiriwa wa Serikali. 

? Awe na elimu ya Shahada ya kwanza katika fani ya Manunuzi na Ugavi (Procurement and Supply Chain/logistic Management) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). 

? Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

 

Utaratibu wa kuwasilisha maombi: Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na maombi yawasilishwe kwa njia ya Posta kwa kutumia anuani ifuatayo:- 

 

MKURUGENZI MWENDESHAJI, 

SHIRIKA LA BIASHARA LA TAIFA ZANZIBAR (ZSTC), 

S. L. P 26 - ZANZIBAR. 

 

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:- 

 

i. Taarifa binafsi za muombaji (CV). 

ii. Vivuli vya vyeti vya kumalizia masomo. 

iii. Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa. 

iv. Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi. 

v. Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa hivi karibuni. 

 

Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 29 June, 2020 wakati wa saa za kazi. 

 

BOFYA HAPA KUPAKUA PDF FILE YA TANGAZO HILI



Download

Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English