Nafasi za Kazi wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar

Maelezo

Chanzo: Utumishi Zanzibar



Tarehe Iliyotolewa: 2018-08-20



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 26445 ... Deadline: 2018-08-24 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kama ifuatavyo:-



IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI:

1.Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 2” 

Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe na elimu ya Stashahada katika fani ya ‘Utunzaji wa Kumbukumbu’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

IDARA YA MAKUMBUSHO NA MAMBO YA KALE:

1.Muhudumu Daraja la III “Nafasi 2” 

Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe ni Mwenye elimu ya Sekondari na kupata cheti.

2.Msaidizi Afisa Makumbusho Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe na elimu ya Stashahada katika fani ya ‘Heritage Management’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

3.Mlinzi Daraja la III “Nafasi 2”

Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Mwenye elimu ya Sekondari na kupata Mafunzo ya Ulinzi (JKU) au (JKT).

IDARA YA HABARI MAELEZO:

1.Mtunza Ghala Daraja la III “Nafasi 1” Unguja 

Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe na elimu ya Stashahada katika fani ya ‘Material Management’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

2.Muhudumu Daraja la III “Nafasi 2” 

Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe ni Mwenye elimu ya Sekondari na kupata cheti.


Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI, S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuiainisha nafasi ya kazi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa. Muombaji anatakiwa aliwasilishe ombi lake MWENYEWE .
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 24 Agosti, 2018 wakati wa saa za kazi.

• Tangazo hili pia linapatikana katika Tovuti WWW.LPS.GO.TZ



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English