Nafasi za Kazi za Wasaidizi wa Sheria kwa Unguja na Pemba
Maelezo
Chanzo: Utumishi Zanzibar
Tarehe Iliyotolewa: 2022-04-22
TANGAZO LA NAFASI ZA WASAIDIZI WA SHERIA KWA UNGUJA NA PEMBA
Posted: 2022-04-22 09:25:29
Afisi ya Rais- Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora kupitia Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria kwa kushirikiana na Shirika la Legal Services Facility (LSF) chini ya program ya Kuimarisha Upatikanaji wa Haki inajiandaa kutekeleza shughuli ya Upatikanaji wa Wasaidizi wa Sheria wataofanya kazi ya kujitolea kupitia Shehia mbali mbali za Unguja na Pemba.
Afisi ya Rais-Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora inakaribisha maombi ya nafasi za Wasaidizi wa Sheria 50 katika majimbo 32 ya Unguja na 18 Pemba kwa waombaji wenye sifa stahili.
SIFA ZA WAOMBAJI
1) (a) Shahada ya kwanza katika fani yoyote kutoka katika taasisi inayotambulika na Serikali, isipokuwa Shahada ya Kwanza ya Sheria;
(b) Cheti au Stashahada kutoka katika taasisi inayotambulika na Serikali; au
(c ) Cheti chochote cha elimu ya Sekondari.
2) Awe ni mkaazi wa Shehia atayoifanyia kazi
3) Awe tayari kujitolea (Ni kazi ya kujitolea na haina mshahara wa kila mwezi); na
4) Awe mwaminifu, mwadilifu na mwenye kukubalika na kuhesimiwa na jamii yake
NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI
Muombaji anatakiwa aandike barua ya maombi na kuambatanisha na mambo yafuatayo: -
(a) Vivuli vya Vyeti vya Kumalizia masomo.
(b) Maelezo binafsi ya Muombaji (CV).
(c) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
(d) Picha moja ya Muombaji (Passport size) iliopigwa karibuni.
(e) Majina na anuani ya Wadhamini wawili wanaotambulika.
(f) Barua ya Sheha ya Shehia anayoishi.
MAMBO YA KUZINGATIWA
i Barua za maombi ziandikwe kwa mkono na ziwasilishwe moja kwa moja kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Upatikanaji wa Wasaidizi wa Sheria.
ii Kwa nafasi za Pemba waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar- Chake-Chake -Miembeni, Mkabala na Benki ya NMB.
iii Siku ya mwisho ya kupokea maombi ni Ijumaa tarehe 29 Aprili, 2022 saa 8.30 Mchana.
iv Mawasiliano yatafanywa kwa wale tu watakaopita katika mchujo wa awali (shortlisted).
Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo
MWENYEKITI,
KAMATI YA UPATIKANAJI WASAIDIZI WA SHERIA,
S.L.P 3360,
KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA,
KIJANGWANI,
ZANZIBAR.
CLICK HERE TO VISIT THE ZANZIBAR UTUMISHI WEBSITE FOR MORE INFORMATION