Nafasi za Kujifunza Lugha Turkey kwa Wafanya kazi wa Umma
Maelezo
Chanzo: Wizara ya Elimu Zanzibar
Tarehe Iliyotolewa: 2024-08-14
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar inatangaza programu ya mafunzo ya lugha ya Kituruki kwa Watumishi wa Umma na Wanataaluma “Turkish Language Program for Public Official and Academicians” – KATIP inayofadhiliwa na Serikali ya Uturuki. Programu hiyo itaendeshwa kwa kipindi cha miezi nane (8) kuanzia Novemba 2024 hadi Julai 2025.
Gharama za ushiriki kwenye mafunzo hayo ikiwa ni Pamoja na ada ya mafunzo, fedha ya kujikimu kila mwezi, tiketi za ndege Kwenda na kurudi, malazi na gharama za usafiri wa ndani zitagharamiwa na Serikali ya Uturuki. Gharama ya bima ya afya ya mshiriki itapaswa kulipiwa na mshiriki mwenyewe.
Taarifa zaidi kuhusu programu hiyo ikiwemo vigezo na namna ya kuwasilisha maombi zinapatikana kupitia tovuti: https://tbbs.turkiyeburslari.gov.tr
Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,
S.L.P 394
Mazizini
Zanzibar.
Barua Pepe: unt.hest@moez.go.tz|hestpemba@moez.go.tz
KWA TAARIFA ZAIDI TEMBELEA LINK HII