Nafasi za kazi 195 Mahakama
Maelezo
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI 195
Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4/2011 inaipa Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na majukumu yake mengine, mamlaka ya kuajiri watumishi wa Mahakama wa kada mbalimbali.
Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapa chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Mahakama ya Tanzania kwenye Mikoa na Wilaya mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi. Nafasi hizo ni Hakimu Mkazi Daraja la II – (TJS 2) nafasi 114, Afisa Utumishi Daraja la II nafasi 3 (TGS D) Katibu Mahsusi Daraja la III – (TGS B) nafasi 6, Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – (TGS B) nafasi 27, Mlinzi (TGOS A) nafasi 27, Msaidizi wa Hesabu (TGS B) nafasi 1 na Msaidizi wa Ofisi (TGOS A) nafasi 17.
TAFADHALI PAKUA PDF FILE KWA MAELEZO ZAIDI