Nafasi za kazi Baraza la Vijana Zanzibar
Maelezo
Chanzo: Utumishi Zanzibar
Tarehe Iliyotolewa: 2017-10-10
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto kwa ajili ya Baraza la Vijana Zanzibar kama ifuatavyo:-
1. Afisa Mipango Daraja la II “Nafasi 2”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Uandishi na Usimamizi wa Miradi au Uchumi au Mipango’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
2. Afisa Uratibu na Ufuatiliaji Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Takwimu au Demographic au Maendeleo ya Jamii’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
3. Afisa Tehama Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘ICT’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
4. Afisa Sheria Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Sheria’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.
• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 13 Oktoba, 2017 wakati wa saa za kazi.