Nafasi za kazi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

Maelezo

Chanzo: Utumishi Zanzibar



Tarehe Iliyotolewa: 2018-07-10



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 12662 ... Deadline: 2018-07-13 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ kama ifuatavyo:-

1. Afisa Usajili wa Wilaya Daraja la II “Nafasi 11” (Nafasi moja kwa kila Wilaya Unguja na Pemba)
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Sheria’ au ‘Utawala’ au ‘Information Technology’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Afisa Usajili Msaidizi Daraja la III “Nafasi 11” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya “Information Technology” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Afisa Tehama Daraja la II “Nafasi 3” - 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya “Computer Science” au “Information Technology” au Computer Networking” au “Computer Engineering kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

4. Takwimu Daraja la II “Nafasi 2” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya “Takwimu” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuiainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 13 Julai, 2018 wakati wa saa za kazi.



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English