Nafasi za kazi Wizara ya Afya

Maelezo

Chanzo: Utumishi Zanzibar



Tarehe Iliyotolewa: 2017-08-18


Download


Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 8240 ... Deadline: 2017-08-25 00:00:00

NAFASI ZA KAZI WIZARA YA AFYA

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Wizara ya Afya kama ifuatavyo:-

1.Afisa Afya Mazingira (Entomology) Daraja la II “Nafasi 1” – Unguja
Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya katika fani ya Afisa Mazingira kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2.Mfamasia Daraja la II “Nafasi 1” - Unguja
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Ufamasia kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Afisa Mionzi Msaidizi Daraja la III “Nafasi 11” - Unguja
Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe na elimu ya Stashahada ya Mionzi (Rediographer) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4) Wauguzi Vijijini (PHN ‘B’) Daraja la III “Nafasi 2” - Unguja
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Cheti katika fani ya Uuguzi Vijijini (PHN ‘B’) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5) Mhandisi Vifaa Tiba Daraja la II “Nafasi 1” - Unguja
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Uhandisi Vifaa Tiba (Biotechnology) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6) Afisa Tabibu Daraja la III “Nafasi 4” - Pemba
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Clinical Officer kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

7)Muuguzi Afya ya Akili (PSY) Nurse Daraja la III “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Uuguzi wa Afya ya Akili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

8)Fundi Sanifu Maabara (Lab Technology) Daraja la II “Nafasi 2” - Pemba
Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Lab Technology kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

9)Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja la III “Nafasi 3” - Pemba
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Afya Mazingira (Environmental Health) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 25 Agosti, 2017 wakati wa saa za kazi.



Download

Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English