Kituo cha Kazi/Tukio: ZanzibarImetembelewa mara! 1621 ... Deadline: 2025-04-05 15:30:00
POST
Afisa Uchumi Daraja la II-UNGUJA - 2 POST
EMPLOYER
OFISI YA MTAKWIMU MKUU WA SERIKALI
APPLICATION TIMELINE:
From: 29-03-2025 To: 05-04-2025
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
Kutoa Ushauri wa masuala ya Kiuchumi kwa Viongozi ili kusaidia kuboresha takwimu za kiuchumi katika Taasisi;
Kufanya Utafiti wa maswala ya Kiuchumi na kutoa mapendekezo ya kisera kwa taasisi;
Kufanya tathmini na Kuchambua Takwimu za Uchumi, Sera za Uchumi pamoja na kutoa taarifa juu ya hali ya uzalishaji wa Takwimu, viashiria vya Maendeleo ya kiuchumi;
Kuandaa Mipango kazi ya Uchumi kwa mwezi, robo mwaka na mwaka kwa kazi za utekelezaji wa Ofisi na kuziwasilisha katika Idara husika;
Kushirikiana na Wadau wa Sekta za Uchumi katika mipango ya utekelezaji wa Sera na mikakati ya kiuchumi ya taasisi;
Kusimamia na Kutekeleza Miradi ya Uchumi pamoja na kutoa ushauri juu ya utekelezaji wa miradi hiyo;
Kuandaa Ripoti za utkelezaji kwa mwezi, robo mwaka na mwaka na kuziwasilisha katika sehemu husika ya taasisi;
Kushiriki katika kuchambua na kutafsiri Takwimu na taarifa mbali mbali za Kiuchumi;
Kufanya kazi nyengine yoyote atakayopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Awe amehitimu elimu ya shahada ya kwanza katika fani ya Uchumi (economics), sayansi ya uchumi au uchumi wa kimataifa katika chuo kinachotambuliwa na Serikali;
Awe na Uwezo mzuri wa kutumia Kompyuta;
Awe na Uwezo mzuri wa uchambuzi wa takwimu za Kiuchumi zinazozalishwa na kukusanywa na Ofisi;