Nafasi za kazi katika Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Unguja na Pemba
Maelezo
Chanzo: Utumishi Zanzibar
Tarehe Iliyotolewa: 2019-06-11
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-
Afisa Ugani Daraja la II “Nafasi 1” Unguja na “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Agriculture Extension” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Afisa Msaidizi Uzalishaji/Tiba Mifugo Daraja la III “Nafasi 2” Unguja na “Nafasi 2” - Pemba
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Stashahada ya Utibabu wa Mifugo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wahudumu Mifugo Daraja la III “Nafasi 3” Unguja na “Nafasi 2” - Pemba
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya elimu ya Sekondari
Walinzi Daraja la III “Nafasi 6” Unguja na “Nafasi 2” - Pemba
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amemaliza elimu ya Sekondari.
Awe amepata mafunzo ya Ulinzi (Mgambo au JKU au JKT)
Afisa Mtafiti Mifugo Daraja la II “Nafasi 3” Unguja na “Nafasi 2” - Pemba
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Udaktari wa Mifugo au Sayansi ya Wanyama au Bioteknolojia kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Afisa Msaidizi Mtafiti Mifugo Daraja la III “Nafasi 7” Unguja na “Nafasi 2” - Pemba
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Uzalishaji Mifugo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wahudumu Shambani Daraja la III Nafasi 12” Unguja na “Nafasi 3” Pemba
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya ya Sekondari.
Afisa Uchumi Kilimo Daraja la II “Nafasi 1” Unguja na “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uchumi wa Kilimo “Economic Agriculture” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Daktari wa Kilimo Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Udaktari wa Wanyama kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jinsi ya Kuomba:
Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.
Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuiainisha nafasi ya kazi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 14 Juni, 2019 wakati wa saa za kazi.