Nafasi za kazi kwa ajili ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Unguja na Pemba

Maelezo

Chanzo: Utumishi Zanzibar



Tarehe Iliyotolewa: 2019-05-24



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 18705 ... Deadline: 2019-05-31 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-

IDARA YA MIPANGO SERA NA UTAFITI:
1. Afisa Miradi Daraja la II “Nafasi 1” - Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mipango kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Afisa Sheria Daraja la II “Nafasi 1” - Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

IDARA YA WATU WENYE ULEMAVU:

1. Afisa Manunuzi Msaidizi Daraja la III “Nafasi 1” – Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Ununuzi na Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

OFISI KUU PEMBA:

1. Afisa Habari Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uandishi wa Habari kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Afisa Utawala Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Utawala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

IDARA YA WATU WENYE ULEMAVU PEMBA:
1. Afisa Uhamasishaji Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Social Work’ au ‘Public Administration’ au ‘Development Study’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


1. Afisa Ufuatiliaji na Tathmini Daraja la II “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uchumi au Mipango au Utawala wa Umma kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

KAMISHENI YA KUKABILIANA NA MAAFA PEMBA:

1. Afisa Utawala Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Utawala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

TUME YA KITAIFA YA KURATIBU NA UDHIBITI WA DAWA ZA KULEVYA PEMBA:

1. Afisa Uchumi na Udhibiti Daraja la II “Nafasi 2” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Mlinzi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amemaliza elimu ya Sekondari.
• Awe amepata mafunzo ya Ulinzi (Mgambo au JKU au JKT)

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA MAZINGIRA:
1. Afisa Utumishi Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Rasilimali Watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Afisa Sheria Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


3. Katibu Muhtasi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Ukatibu Muhtasi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Mlinzi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amemaliza elimu ya Sekondari.
• Awe amepata mafunzo ya Ulinzi (Mgambo au JKU au JKT)

5. Taarishi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari na kufaulu.

6. Mwangalizi wa Ofisi Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utawala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

7. Dereva Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Cheti cha Udereva na leseni hai ya udereva kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. 

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 31 Mei. 2019 wakati wa saa za kazi
 



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English