Nafasi za kazi wizara ya Afya Zanzibar
Maelezo
Chanzo: Utumishi Zanzibar
Tarehe Iliyotolewa: 2017-11-24
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara Afya – Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-
1. AFISA MAABARA DARAJA LA II - Nafasi moja (1) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Maabara mwenye Shahada ya pili ya “Science in Immunology” atapewa kipaumbele kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
2. MTAALAMU WA VIUNGO BANDIA DARAJA LA II – Nafasi moja (1) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe mzanzibari
• Awe na shahada ya kwanza ya teknolojia ya maabara na viungo bandia (Prosthenics and orthotics)-
3. DAKTARI WA WANYAMA DARAJA LA II – Nafasi moja (1) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza ya Udaktari wa Wanyama kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
4. WAUGUZI DARAJA LA III – Nafasi kumi (10) Unguja na Nafasi ishirini (20) Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Uuguzi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
5. AFISA TABIBU DARAJA LA III – Nafasi tano (5) Unguja na Nafasi kumi (10) Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Utabibu (Clinical Medicine) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
6. FUNDI SANIFU MADAWA DARAJA LA III – Nafasi saba (7) Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Famasia (Phamaceutical technician) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
7. AFISA USHAURI NASAHA DARAJA LA II – Nafasi tatu (3) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza ya Ushauri nasaha kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
8. FUNDI SANIFU MAABARA MSAIDIZI DARAJA LA III – Nafasi tano (5) Unguja na Nafasi tisa (9) Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Maabara kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
9. AFISA MAZINGIRA MSAIDIZI DARAJA LA III – Nafasi mbili (2) Unguja na Nafasi nane (8) Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Afya ya Mazingira kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
10. AFISA UCHUMI AFYA (HEALTH ECONOMIST) DARAJA LA II – Nafasi mbili (2) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na shahada ya kwanza ya uchumi wa afya.
11. AFISA RASILIMALI WATU DARAJA LA II – Nafasi mmoja (1) Unguja na Nafasi mmoja (2) Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
12. AFISA UHUSIANO DARAJA DARAJA LA III – Nafasi mmoja (1) Unguja na Nafasi mmoja (1) Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza Uhusiano wa Umma “Public Relation” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
13. AFISA MIPANGO UTUMISHI DARAJA LA II – Nafasi mbili (2) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza ya Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
14. AFISA UTAWALA DARAJA LA II – Nafasi mbili (2) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza ya Utawala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
15. AFISA HABARI MSAIDIZI DARAJA LA III – Nafasi moja (1) Unguja Nafasi moja (1) Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya uandishi wa habari kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
16. AFISA USTAWI WA JAMII MSAIDIZI DARAJA LA III – Nafasi nne (4) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Ustawi wa Jamii kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
17. AFISA MANUNUZI DARAJA LA II – Nafasi nne (4) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza ya Manunuzi na Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
18. KATIBU MUHTASI DARAJA LA III – Nafasi tatu (3) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Uhazili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
19. DEREVA DARAJA LA III – Nafasi tano (5) Unguja Nafasi nne (4) Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Cheti cha Udereva na leseni ya Udereva Class “C” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
20. KARANI MAPOKEZI DARAJA LA III – Nafasi mbili (2) Unguja Nafasi moja (2) Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Cheti cha Mapokezi (Castermer Care) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
21. WALINZI DARAJA LA III – Nafasi tatu (3) Unguja Nafasi tatu (3) Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari pamoja na Cheti cha Mafunzo ya Ulinzi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
22. DOBI DARAJA LA III – Nafasi moja (2) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari pamoja na Cheti cha Mafunzo ya Udobi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
23. MTUNZA BUSTANI DARAJA LA III – Nafasi moja (1) Unguja Nafasi mbili (2) Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari.
24. MPISHI DARAJA LA III – Nafasi mbili (2) Unguja Nafasi mbili (2) Pemba.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Cheti cha Upishi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
25. MSHONI DARAJA LA III – Nafasi moja (1) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Cheti cha Ushoni kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
26. FUNDI BOMBA DARAJA LA III – Nafasi mbili (2) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Cheti cha Ufundi Bomba kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
27. AFISA UFUATILIAJI NA TATHMINI DARAJA LA II – Nafasi mbili (2) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza ya Uchumi au Mipango kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
28. MTAALAMU WA MIONZI – Nafasi kumi (10) Unguja na Pemba
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza au Stashahada ya Mionzi (Radigrapher) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
29. AFISA HABARI NA MAWASILIANO DARAJA LA II – Nafasi tatu (4) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Computa, Habari na Mawasiliano “ICT” au Uhandisi wa Komputa “Computer Engineering” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
30. FUNDI UMEME DARAJA LA III – Nafasi nne (4) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Ufundi Umeme kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
31. MUHANDISI UMEME DARAJA LA II – Nafasi moja (1) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza ya Uhandisi Umeme kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
32. FUNDI SEREMALA DARAJA LA III - Nafasi moja (1) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Ufundi Seremala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
33. MUHUDUMU AFYA DARAJA LA III - Nafasi moja (11) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari.
34. DRAIN BOY (MZIBUA KARO) DARAJA LA III - Nafasi moja (1) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari.
35. FUNDI MUASHI DARAJA LA III - Nafasi moja (1) Unguja.
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Cheti cha Ufundi Muashi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S.L.P 1587 - ZANZIBAR.
• Muombaji anaweza kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini wakati wa saa za kazi.
• Kwa Waombaji walioko Pemba wanaweza kuwasilisha maombi yao katika Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma iliopo Chake Chake – Pemba.
• Aidha muombaji anatakiwa aanishe nafasi ya kazi anayoiomba miongoni mwa zilizotajwa hapo juu.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo.
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size ilizopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 30 Novemba, 2017 wakati wa saa za kazi.