Tangazo la Nafasi ya Kazi Mhandisi Madini Daraja la Pili

Maelezo

Chanzo: ZanAjira



Tarehe Iliyotolewa: 2023-01-13



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 29032 ... Deadline: 2023-01-26 04:46:00

POSTMHANDISI MADINI DARAJA LA II - UNGUJA - 1 POST
EMPLOYERWIZARA YA MAJI NISHATI NA MADINI
APPLICATION TIMELINE:From: 11-01-2023 To: 26-01-2023
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
  1. Kuratibu shughuli zote za Migodi na Madini Zanzibar ikiwa ni pamoja na uingizaji na usafirishaji wa madini nje ya nchi;
  2. Kusimamia tafiti za kijiolojia za Madini katika eneo lote la Zanzibar;
  3. Kuandaa, kusimamia na kutathmini sera na sheria ya madini ya Zanzibar pamoja na mipango kazi yake;
  4. Kuandaa mifumo ya kisheria na ya kitaasisi ili kukuza uwekezaji katika sekta ya madini;
  5. Kushajihisha uwekezaji wa sekta binafsi katika sekta ya madini pamoja na kujenga uwezo wa uongezaji thamani wa madini;
  6. Kushirikiana na Mamlaka za madini za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kudhibiti utoroshaji wa madini nje ya nchi;
  7. Kubuni vyanzo vipya vya mapato yatokanayo na madini;
  8. Kufanya mashirikiano ya kikanda na ya kimataifa kuhusiana tafiti za kijiologia (Geological Research);
  9. Kujenga uwezo wa ndani ya nchi katika kushughulikia sekta ya madini na kuchangia katika uchumi ikiwemo kutayarisha wataalamu na kuwatunza katika taasisi za ndani;
  10. Kuimarisha ushiriki wa ndani katika sekta ya madini;
  11. Kudhibiti biashara ya madini.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE
  1. Awe Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka 46.
  2. Awe mwenye Shahada ya Kwanza ya Uhandisi Madini kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali
REMUNERATIONZPSG - 08

 Kwa maelezo zaidi unaweza kufuata link https://bit.ly/3kgkO9v



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English