nafasi kumi na nne (14) za kazi kwa ajili ya Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar

Maelezo

Chanzo:



Tarehe Iliyotolewa: 2021-08-28



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 15977 ... Deadline: 2021-09-03 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi kumi na nne (14) za kazi kwa ajili ya Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-

1. Afisa Mpimaji Ardhi Daraja la II “Nafasi 4” Unguja na “Nafasi 2 - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Upimaji (Geomatics au Geoinformatics) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Afisa Ardhi Daraja la II “Nafasi 3” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Usimamizi wa Ardhi (Land Management and Valuation, Real Estate) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Afisa Mkadiriaji Majengo Daraja la II “Nafasi 2” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Ukadiriaji Majengo (Quantity Surveying) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Afisa Mipango Miji Daraja la II “Nafasi 3” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Sayansi ya Mipango Miji (B.S in Urban and Regional Planning au B.S. in Regional Development Planning) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Sheria House Mazizini Zanzibar katika Ghorofa ya sita (6) wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini – Gombani. 

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 03 Septemba, 2021 wakati wa saa za kazi



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English