Nafasi za Ufadhili wa Ada M.A Kiswahili UDSM
Maelezo
CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
TAASISI YA TAALUMA ZA KISWAHILI
UFADHAILI WA MASOMO YA MA KISWAHILI
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya ALAF Limited inafuraha kuwatangazia ufadhili wa ada kwa wanafunzi watatu (3) waliochaguliwa kusoma Programu ya M.A Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa mwaka wa masomo 2020/2021. Mwaombaji awe na sifa zifuatazo:
1. Raia wa Tanzania,
2. Mhitimu wa BA Kiswahili,
3. Awe na wakia (GPA) usiopungua 3.8 wa Digrii ya Kwanza,
4. Awe amepata Udahili wa M.A Kiswahili CKD,
5. Umri usiozidi miaka 30 wakati analeta maombi,
6. Awe ni muhitaji wa ufadhili wa ada,
7. Awe na uwezo wa kujigharimia mahitaji mengine (chakula, steshenari, malazi, utafiti n.k).
Nyaraka Muhimu za Kutuma
1. Barua ya maombi ambayo pia itabainisha uwezo wako wa kitaaluma,
2. Nakala ya cheti cha Matokeo ya Kitaaluma ya Shahada ya kwanza (Transcript),
3. Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa,
4. Maelezo mafupi (Ukurasa mmoja) kueleza kwa nini unahitaji ufadhili wa ada.
Maombi yatumwe kwa: Mkurugenzi, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili Baruapepe: iks@udsm.ac.tz Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 11/11/2020.