Nafasi za kazi TEMESA, Wizara ya Afya, Wizara ya Ardhi na Kwengineko

Maelezo

Chanzo: Utumishi TanzaniaTarehe Iliyotolewa: 2021-06-17Kituo cha Kazi/Tukio: Tanzania/USA
Imetembelewa mara! 31195 ... Deadline: 2021-07-01 15:30:00

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/L/144 17 Juni, 2021 TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mtendaji Mkuu Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), Katibu Mkuu Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Katibu Mkuu Wizara ya Maji anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi sitini na nne (64) kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.

1.0 MWAJIRI: MTENDAJI MKUU WAKALA WA UFUNDI NA UMEME TANZANIA

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) ni Wakala chini ya Wizara ya Ujenzi ulioanzishwa chini ya mamlaka ya sheria ya wakala za serikali Na. 30 ya mwaka 1997 kwa amri ya serikali na Waziri wa Ujenzi kupitia tangazo la serikali Na. 254 la tarehe 26 Agosti 2005, kuchukua majukumu ambayo hapo awali yalifanywa na Kitengo cha Umeme na Mitambo (E&M) cha Idara chini ya Wizara ya Ujenzi iliyokuwa na ari ya kuboresha huduma na kuongeza tija na ufanisi. TEMESA ilianzishwa mahususi kutoa huduma za Umeme, Mitambo na Elektroniki, Huduma za vivuko pamoja na Ukodishaji Mitambo kwa taasisi za serikali na Umma kwa jumla.

 

TAFADHALI PAKUA FAILI LA PDF HAPA KWA MAELEZO ZAIDIShare via Whatsapp

Advertise a product

©2022 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English