Nafasi za Kazi Kwa kada za Sheria Zanzibar

Maelezo

Chanzo: Utumishi SMZTarehe Iliyotolewa: 2022-09-21Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 25144 ... Deadline: 2022-09-28 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi ya AFISA SHERIA DARAJA LA II na KARANI SHERIA DARAJA LA III kama ifuatavyo:- 

1.AFISA SHERIA DARAJA LA II: Katika Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo :- 

1.Ofisi ya Rais, Ikulu - Unguja “Nafisi 1” na Pemba “Nafasi 1” 
2.Afisi ya Mwanasheria Mkuu - “Nafasi 8” 
3.Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka - “Nafasi 10” 
4.Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma - “Nafasi 2” 
5.Wizara ya Maji, Nishati na Madini- Pemba - “Nafasi 1” 
6.Tume ya Utumishi Serikalini - “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji: 
?Awe ni Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka aroubaini na sita (46). 
?Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
?Asiwe muajiriwa wa Serikali. 

2.KARANI WA SHERIA DARAJA LA III: Katika Afisi ya Mwanasheria Mkuu. 

Sifa za Waombaji: 
?Awe ni Mzanzibari mwenye umri usiopungua miaka aroubaini na sita (46). 
?Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
?Asiwe muajiriwa wa Serikali. 

Jinsi ya Kuomba: 
?Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa Kielektronic wa maombi ya ajira (Zanajira) kupitia anuani ifuatayo:- http://portal.zanajira.go.tz kuanzia tarehe 14 Septemba, 2022 hadi tarehe 28 Septemba, 2022. 

?Mfumo huo pia unapatikana katika tovuti ya Tume ya Utumishi Serikalini www.zanajira.go.tz 

?Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo:- 

KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI, 
S.L.P. 1587, 
ZANZIBAR. ? Muombaji anatakiwa kuanisha nafasi ya kazi aliyoombea 

Kwa msaada wa kitalamu wasiliana na Tume ya Utumishi Serikalini kupitia email: helpdesk@zanajira.go.tz au Simu Nam. 0773101012. 

TANBIHI: 
Tume ya Utumishi Serikalini inawatahadharisha waombaji wote kwamba ajira zinatolewa bure. Hivyo, wanatakiwa kujiepusha na Matapeli wanaotumia nafasi hizi kwa kujipatia kipato kisicho cha halali. 
 

 

Click here to Apply

Click here to go to utumishi website
 Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English