Nafasi za kazi SMIDA
Maelezo
WAKALA WA MAENDELEO YA VIWANDA VIDOGO VIDOGO, VIDOGO NA VYA KATI (SMIDA)
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Wakala wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo, Vidogo na vya Kati (SMIDA) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria No.2 ya mwaka 2018.
Kwa mujibu wa sheria ya hiyo, Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala ina mamlaka ya kuajiri wafanyakazi wa Wakala kwa mujibu wa kifungu Namba 5(g) cha Sheria ya Wakala Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo, Vidogo na vya Kati.
Hivyo, Wakala wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo, Vidogo na vya Kati (SMIDA) inakaribisha maombi ya kujaza nafasi tupu katika Kada mbali mbali kwa waombaji wenye sifa stahili katika Ofisi yake iliyopo Maruhubi Unguja na Pujini Chake Chake Pemba.
Nafasi zenyewe ni kama zifuatazo;
UNGUJA
1. MHANDISI MITAMBO DARAJA LA II (ZPSG-08) nafasi moja
Sifa za muombaji
? Awe ni Mzanzibari.
? Awe na Shahada ya kwanza katika fani ya Uhandisi Mitambo (Bachelor of Engineering in Mechanical Engineering) au Mitambo na Elektroniki (Bachelor of Egineering in Mechatronic Engineering) au fani nyingine inayolingana nayo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.