Kituo cha Kazi/Tukio: TANZANIAImetembelewa mara! 18957 ... Deadline: 2023-02-16 23:54:00
POST
MUHANDISI VIFAA TIBA (BIOMEDICAL ENGINEER) DARAJ LA II - 5 POST
EMPLOYER
WIZARA YA AFYA
APPLICATION TIMELINE:
From: 28-01-2023 To: 16-02-2023
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
Kuratibu uaandaji wa sifa za vifaa (technical specification), ununuzi, ufungaji (installation), ukarabati, ugezi (calibration) na kuthibitisha vifaa tiba.
Kuweza kuthibitisha vifaa vipya kwa kufanya majaribio, kuhakikisha vinafanyakazi kama ilivyotarajiwa na kufanya mabadiliko yanayotakiwa.
Aweze kutoa ushauri kwa uongozi wa Hospitali kuhusu vifaa tiba.
Kutunza vifaa kwa kufanya ukarabati wa awali (preventive maintenance) na kuweka ratiba ya matengenezo.
Kuitisha matengenezo ya vifaa ikiwa ni pamoja na kupitia mikataba ya huduma na kusimamia matengenezo hayo.
Kupokea, kuhifadhi pamoja na kusambaza vifaa tiba pamoja na kutunza kumbukumbu.
Kusimamia matumizi sahihi ya vifaa kwa watumiaji ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri wa kitaalam juu ya matumizi bora ya vifaa hivyo.
Kuandaa ripoti ya ufuatiliaji wa vifaa kwa kukusanya, kuchambua na kufupisha taarifa na mwenendo wa vifaa tiba.
Kuhakikisha uwepo wa mazingira salama ya ufanyaji kazi kwa kufanya majaribio ya kiusalama (safety test), kushauri na kuafikiana na miongozo, mafunzo na kuwaelekeza watumiaji kufuata kanuni za kiusalama.
Kuandaa bajeti ya huduma za matengenezo ya vifaa tiba
Kuagiza vipuri vya vifaa tiba.
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Awe ni Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka arobaini na sita.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya “Biomedical Engineering” au “Biomedical Technology” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.