Nafasi za Kazi Wizara ya Elimu Zanzibar

Maelezo

Chanzo: Utumishi ZanzibarTarehe Iliyotolewa: 2017-11-19Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 6232 ... Deadline: 2017-11-24 00:00:00

 Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali - Pemba kama ifuatavyo:-

1. WALIMU WA SANAA NGAZI YA CHETI - Nafasi thamanini na saba (87)
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu mafunzo ya Ualimu wa Sanaa ngazi ya Cheti katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
2. WALIMU WA SAYANSI NGAZI YA CHETI – Nafasi kumi na sita (16)
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu mafunzo ya Ualimu wa Sayansi ngazi ya Cheti katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. WALIMU WA SANAA NGAZI YA STASHAHADA – Nafasi ishirini na nane (28)
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu mafunzo ya Ualimu wa Sanaa ngazi ya Stashahada katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. WALIMU WA SAYANSI NGAZI YA STASHAHADA – Nafasi tisa (9)
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu mafunzo ya Ualimu wa Sayansi ngazi ya Stashahada katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. WALIMU WA SANAA NGAZI YA SHAHADA YA KWANZA – Nafasi sita (6)
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu mafunzo ya Ualimu wa Sanaa ngazi ya Shahada ya kwanza katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6. WALIMU WA SAYANSI NGAZI YA SHAHADA YA KWANZA – Nafasi tano (5)
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu mafunzo ya Ualimu wa Sayansi ngazi ya Shahada ya kwanza katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S.L.P 1587 - ZANZIBAR.
• Muombaji anaweza kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini wakati wa saa za kazi.
• Kwa Waombaji walioko Pemba wanaweza kuwasilisha maombi yao katika Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma iliopo Chake Chake – Pemba.
• Aidha muombaji anatakiwa aanishe nafasi ya kazi anayoiomba miongoni mwa zilizotajwa hapo juu.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
g) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo.
h) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
i) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
j) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
k) Picha moja (1) ya Passport Size ilizopigwa karibuni.
l) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 24 Novemba, 2017 wakati wa saa za kazi Share via Whatsapp
Advertise with us

©2023 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English