Nafasi za Kazi wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar

Maelezo

Chanzo: Utumishi ZanzibarTarehe Iliyotolewa: 2017-11-19Kituo cha Kazi/Tukio: Pemba
Imetembelewa mara! 8303 ... Deadline: 2017-11-24 00:00:00

 Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara Biashara, Viwanda na Masoko - Pemba kama ifuatavyo:-

1. AFISA BIASHARA NA MASOKO MSAIDIZI - Nafasi mbili (2)
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Usimamizi wa Biashara (Bussness Administration) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. AFISA MANUNUZI MSAIDIZI – Nafasi moja (1)
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Ununuzi na Ugavi (Procurement and Supply) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. MUHUDUMU – Nafasi moja (1)
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na amehitimu elimu ya Sekondari.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S.L.P 1587 - ZANZIBAR.
• Muombaji anaweza kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini wakati wa saa za kazi.
• Kwa Waombaji walioko Pemba wanaweza kuwasilisha maombi yao katika Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma iliopo Chake Chake – Pemba.
• Aidha muombaji anatakiwa aanishe nafasi ya kazi anayoiomba miongoni mwa zilizotajwa hapo juu.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo.
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size ilizopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 24 Novemba, 2017 wakati wa saa za kazi Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English