Nafasi za Kazi Ofisi ya Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe

Maelezo

Chanzo: Utumishi ZanzibarTarehe Iliyotolewa: 2018-02-13Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 8842 ... Deadline: 2018-02-19 00:00:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Ofisi ya Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe kama ifuatavyo:-

1. Fundi Mchundo Daraja la III “Nafasi 2” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Civil Engineer kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

2. Mwandishi wa Miradi Daraja la II “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uandishi wa Miradi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

3. Mwanahistoria Daraja la II “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Historia kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Fundi Umeme Daraja la III “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Ufundi wa Umeme kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Fundi Seremala Daraja la III “Nafasi 2” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Ufundi Seremala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 19 Februari, 2018 wakati wa saa za kazi.Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English